The August
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 1,080
- 2,026
Magufuli Ana Hofu Kubwa Kuwa Kuungana kwa Zitto Na Maalim Seif Kwaweza Kumng'oa 2020
Majasusi hutegemea sana hisia ya sita ((6th sense) katika kufanya baadhi ya maamuzi yao. Na hisia ya sita ilinituma kutowaandalia na kuwatumia #BaruaYaChahali kwa sababu nafsi ilikuwa ikinitaka nisubiri. Awali nilipanga kuandika kuhusu jinsi CCM ya Magufuli ilivyokumbwa na kiwewe baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad aka Maalim Seif kuamua kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe.
Miongoni mwa hofu alizonazo Magufuli na washauri wake huko CCM ni uwezekano wa Zitto na Maalim Seif kupata sapoti ya Waislamu kwa sababu moja ya msingi: tofauti na watangulizi wake - Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete - ambao walijitahidi japo kinafiki kuepuka ubaguzi wa kidini, Magufuli anaangaliwa na wengi kama kiongozi anayewabagua Waislamu waziwazi.
Sina hakika kama yeye binafsi ni mbaguzi dhidi ya Waislamu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba anaendekeza ukanda na ukabila, na kwa vile wateule wake wengi ni watu wa kutoka Kanda ya Ziwa ambayo ina idadi ndogo ya Waislamu, indirectly ukanda/ukabila huo unapelekea ubaguzi wa kidini. Hili halihitaji kuwa jasusi kama mie kulielewa.Lipo wazi. Jihangaishe kuangalia wateule wa Magufuli hususan ngazi ya mikoa na wilaya, hutoshindwa kubaini kuwa kuna tatizo linaloweza kuugharimu umoja na mshikamano wa taifa letu.
Panapo majaliwa mwaka huu nitahitimu shahada ya uzamifu ambayo mada ya utafiti inahusu - pamoja na mambo mengine - manung’uniko ya muda mrefu miongoni mwa Waislamu nchini Tanzania kuwa wanabuguliwa katika nyanja za elimu na ajira. Nisingependa kuingia kwa undani katika hilo hapa kwa sababu sio mahala mwafaka ila tuna tatizo ambalo kwa bahati mbaya sio tu limekuwa likikwepwa na watawala wetu waliotangulia bali pia limefikia pabaya katika Awamu hii ya Tano ya Magufuli.
Turejee kwenye “hisia yangu ya sita.” Hatimaye jana jioni nikafahamu kwanini nafsi ilikuwa inanituma kuvuta subira kabla ya kuwatumia Barua hii. Katika pitapita zangu huko mtandaoni nikakutana na barua kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwenda kwa ACT-Wazalendo ikieleza nia ya msajili huyo kukifuta chama hicho.
Huyu ndio Magufuli. Hii barua ni maelekezo aliyotoa Magufuli kwa msajili wa vyama vya siasa kwa ajili ya utekelezaji. Ni kama maagizo aliyotoa kuhusu Tundu Lissu kwa ajili ya utekelezaji, na nyote mwajua kilichomkumba mbunge huyo wa Chadema. Msishangae pindi Msajili akitekeleza tishio hilo la kuifuta ACT-Wazalendo, sio kwa sababu hizo za kipuuzi zilizobainishwa kwenye barua hiyo bali kwa sababu Msajili huyo anapaswa kutekeleza maagizo ya bosi wake, yaani Magufuli.
Kwanini Magufuli anajaribu mkakati huu hatari? Kuna sababu kuu mbili.
Ya kwanza ni hiyo niliyowaeleza kuwa anawahofia Maalim Seif na Zitto, lakini ya pili ni kwamba “alilamba asali, sasa anachonga mzinga.” Ni kwamba, licha ya
kuzuwia Bunge Live,
kuharamisha shughuli halali za vyama vya upinzani,
kudhibiti vyombo vya habari
kumruhusu mwanae Bashite avunje sheria atakavyo huku akihatarisha maisha ya Watanzania kwa kutumia #WatuWasiojulikana,
kufanya teuzi kwa misingi ya ukanda/ukabila na udini,
kuhujumu vyama vya upinzani kwa kununua wabunge na madiwani (hii ni mada ya siku nyingine kwa sababu nina majina ya wabunge kadhaa wa Chadema walio mbioni kujiunga na CCM baada ya “kukabidhiwa chao”),
kuhusika katika ufisadi kama wa Shilingi trilioni 1.5 huko Hazina (ambako mpwa wake ndio mlipaji mkuu wa fedha za umma), ufisadi ambao baadaye ulibainika kuwa ni wa shilingi trilioni 2.4, sambamba na ufisadi wa mradi wa hati za kusafiri za kielektroniki, ufisadi unaomhusisha pia Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dkt Modestus Kipilimba,
kudharau taratibu za kisheria zinazotaka matumizi ya serikali kupata idhini ya bunge na badala yake anajenga kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwake bila ruhusua ya bunge, sambamba na “kumwaga” fedha kwenye miradi yake mikubwa ya maendeleo (wazo zuri) pasipo kupata ridhaa ya bunge (uvunjifu wa sheria)
changa la macho la mahakama ya ufisadi
kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na Simon Kanguye,
kutekwa Mo Dewji, Roma Mkatoliki
jaribio la kumuua Tundu Lissu
yanayofichwa kuhusu kilichojiri MKIRU
na mengineyo mengi yasiyopendeza
hakujawa na jitihada zozote zakumfikishia ujumbe dikteta huyo kuwa Watanzania hawaafikiani nae. Magufuli anaona kuwa Watanzania wanafikiana nae katika azma yake ya kuibomoa Tanzania. Kwahiyo anaamini kuwa hata akiiangamiza ACT-Wazalendo, hakuna madhara yoyote kwake kama ambavyo ishu hizo nilizotaja hapo juu hazijawa na madhara yoyote kwake.
Kwenye kichwa cha habari cha barua hii nimetanabaisha kuwa kuna watu wanaohusika na hujuma dhidi ya ACT-Wazalendo. Nitawataja baadhi.
Mkurugenzi Mkuu wa TISS Kipilimba ameandaa operesheni malum ya “kuiangamiza ACT-Wazalendo” inayosimamiwa na namba mbili wake aitwaye Nyaulingo.
Wahusika wengine ni pamoja na waandamizi kadhaa huko Bungeni, Ikulu na katika wizara kadhaa. Pia kuna wabunge watatu wa Chadema, mmoja ni afisa kamili wa TISS, na mwingine amekuwa akitajwatajwa kujiunga na CCM, na mbunge mdada machachari. Msaidizi mmoja wa Magufuli anaitwa Majuva (ambaye pia ni mtu wa Kitengo) ndiye anayeratibu “habari chafu” kuhusu Zitto, Maalim Seif na ACT-Wazalendo kwenye magazeti ya Musiba.
Pamoja na mambo mengine, miongoni mwa mikakati ni pamoja na kuwatumia baadhi ya vijana wa Chadema kuzunguka mitandaoni wakipotosha kuwa “muungano” wa Maalim Seif na Zitto ni kazi ya kitengo ili kuibomoa Chadema. Ukizunguka mitandaoni hutoshindwa kumbaini kijana anayeongoza genge hilo.
Nihitimishe kwa kuamini kuwa both Zitto na Maalim Seif ni wanasiasa wakomavu wanaoweza kukabiliana na hujuma za aina yoyote ile. Wito wangu kwao, badala ya kuamini “kirahisi” taarifa hii, wafanye uchunguzi wao kubaini ukweli, na kisha kuchukua hatua watakazoona zinafaa. Mjumbe hauwawi!
Kingine ni ushauri wangu kwa Bwana Zitto kuwa “asirudie kosa la Chadema kwa Lowassa” hasa baada ya kukutana na habari hii huko Jamii Forums.
Sent using Jamii Forums mobile app