Hujafa Hujaumbika-Biashara ni Mapambano

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,655
6,004
Habari za wakati huu;
Ni muda mrefu sana sijaweka andiko katika Jukwaa letu hili pendwa ambalo lina wachangiaji wachache.Nikiri tu kwamba ni kwa sababu mbalimbali sijaweza kuweka andiko hapa haswa kutokana na changamoto mbalimbali za kibiashara na kimaisha.Kama ilivy kawaida yangu huwa napenda kujaribu aina mbalimbali ya Biashara na kwa kweli katika kipindi kirefu kilichopita niliingia katika aina tofauti ya Biashara ambayo nitaaita uwekezaji.Ndio nilihama katika kuwa mfanya biashara anayeuza bidhaa na huduma na kuwa mfanya biashara anayeuza na kununua mtaji.Sikuacha baadhi ya shughuli nilizokuwa nafanya na wala sikubadilisha mfumo wangu wa ufanyaji kazi.Lakini nilibadilika na kujaribu bahatri yangu katika uwekezaji.

Kiuhalisia sikuwa na ukwasi(utajiri) mkubwa wa kuweza kuwa mwekezaji mkubwa anayetengeneza Faida hivyo basi kwa kiwango kukubwa nilitumia kamtaji kango kadogo kufanya uwekezaji katika kampuni kwenye soko la hisa la Dar es Salaam na Fedha nyingine niliwekeza katika kampuni za watu binafsi ambao nilifhamiana nao na kwenye kampuni nyingine niliwekeza muda na ujuzi wangu kidogo kwa kiwango kidog cha umiliki katika kampuni hizo.Kwa mchanganuo tu asilimia 40 ya mtaji wangu niliokuwa nao niliwekeza kwenye soko la Hisa na DSE asilimia 60 nyingine iko kwenye kampuni binafsi ambazo haziko kwenye soko la hisa.

Katika kampuni hizi binafsi ambazo mimi nilikuwa kama Sehemu ya wajumbe na Pia kama mshirikia katika baadhi ya shughuli za utendaji nilijifunza kwamba Faida niyokuwa ninapata ilikuwa kubwa kuliko faida niliyokuwa ninapata katika SOKO la hisa.Ingawa kwenye Soko la hisa Usalama wa Pesa yangu nauona uko JUU lakini kwenye kampuni Binafsi niliona usalama wa Pesa yangu ukiwa mdogo hata hivyo faida niliyopata ilikuwa ni nzuri zaidi.Ili kujilinda kuna Mbinu nilitumia ikiwamo kuwa na Debentures kwenye baadhi ya kampuni nilizoweka Pesa zangu hasa zile za Binafsi huku nikiwa ni sehemu ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.Kwa sababu hiyo nilijifunza pia kuhusu aina mbalimbali za biashara ambazo nisingeweza kujifunza mwenyewe.

Hata hivyo katika Kufanya Shughuli hizi nilijifunza mambo mengi sana ambayo mengine niliyafahamu kabla na mengine sikuwahi kuyaona yakifanyika moja kwa moja.Baadhi ya mambo hayo ndio ambayo yamenifanya niandike Uzi Huu:
  1. Kwanza hakuna biashara ambayo hailipi.Biashara zote zinalipa cha muhimu ni utambue wateja wako ni wapi na uwezo wao wa kulipa ni upi.
  2. Pili nilijifunza kwamba Cashflow is Kingi(Yaani Biashara yenye Mzunguko Mkubwa ndio Biashara)Haijalishi una casha kiasi gani,mtaji mkubwa kiasi gani ila kama Pesa yako haizunguki lazima utafute namna ya kuizungusha
  3. Tatu nikajifunza kwamba Mtaji Sio Pesa.Mtaji ni kila ambacho unaweza kupata kwa kutumia Pesa.Hivyo basi Unapofikiria kuhusu Mtaji Fikiria namna ambavyo uanweza kuvipata vile unavyohitaji bila kutumia Pesa ili uounguze mahitaji ya Pesa kwenye Biashara yako.Hii upunguza Pressure kwenye Mzunguko wako wa Pesa
  4. Nne nilijifunza kwamba (Your Network is Your Networth) wekeza katika kutengeneza mtandao wako na watu unaofahamiana nao.Fahamiana na watu wenye Pesa,wenye maarifa,wenye taarifa,wenye fursa na wenye Mtandao mpana.Hakikisha kwamba mtandao wako unakuwa Mkubwa ila usiwe mtandao ambao unakugharimu sana wewe katika kuwa nao.
  5. Tano nilijifunza kwamba Ni lazima mtu yeyote ambaye ana mpango wa kuwa Tajiri na mwenye ukwasi mkubwa awe na Kmapuni ambayo ni LIMITED na awe na TRUST FUND ambayo itahifadhi mali zake ili zisiathiriwe pale mambo yanapoenda mrama.Ni lazima awe na bima kwa kila aina ya majanga yanayoweza kutokea na ni lazima awe tayari kudaiwa na kudai.
  6. Sita nilijifunza kwamba ni muhimu sana kuwa na Benki inayotambulika.Kwani Benki ina uwezo wa kuzalisha Pesa.Ili kumiliki Benki unaweza kuanza na Kumiliki SACCOS.Ndio SACCOS ni Benki na kama unahitaji utajiri ni lazima UMILIKI BENKI maana kupitia BENKI ni rahisi sana KUPATA PESA
  7. Saba niljifunza Pia kuhusu umuhimu wa Kuwa na mfumo wa Soko UNaojitegemea(Closed Market System) Kwa mfano manweza kuwa na kikundi cha watu ambao mnazalisha bidhaa ambazo nyie ndio watumiaje wake)Kwa mfano kua anayezalisha matunda,mwigine nafaka,mwingine,mboga,mwingine nguo,mwingine vitu vingine.Ambao katika huo mfumo wenu hela inazunguka humo ndani tu na inatoka nje tu pale panmapokuwa na ulazima ila kuingia mnaruhusu hela iingie.Kwa mfano kama nyiye ni wanywaji wa Gambe mnakuwa na Pub ambayo inamilikiwa na mmoja wenu.Na yule wa Pub anakuwa ananunua Sehemu ya Jumla inayomilikwa na mmoja wenu an ikiwezekana mmoja wenu awe na kiwanda kabisa cha Gambe ili mhakikishe kwamba Pesa inayotoka kwenye Mtandao wenu ni ndogo zaidi kuliko ile inayoingia(Balance of Trade)
Haya ni baadhi ya madini ambayo nimejifunza kwa muda ambao nimekuwa mbali na ninyi na nilikuwa Jukwaani kwani ni eneo langu la kujidai.Kama unahitaji Mjadala zaidi kuhusu haya niliyoandika hapa usisite kuwasiliana nasi kwa emails:masokotza@gmail.com au masokotz@yahoo.com.

Nawatakieni kila la heri katika mapambano yenu
 
Asante sana kwa andiko zuri. Naomba unipe uzoefu wako kwa kampuni hizi binafsi zizazo supply mahitaji/bidhaa mbalimbali kwa taaisis za Serikali lakini malipo unakuta yanachelewa sana meanwhile bado wana kwambia wanahitaji bidhaa! Hii unafanyaje kuepuka kufiliska. Maana hela unaitaka lakini hailipwi kwa wakati. Meanwhile kodi ziko pale pale + operation cost+ other utilities.
 
Mkuu,NI changamoto.Kwanza hakikisha unao mkataba wao na uone masharti yao yanasemaje.Kwa sababu kimsingi iwapo wamechelewesha Malipo kuna taratibu za kimakataba na za kibiashara ambazo unaweza kuzitumia.Cha muhimu ni kufahamu tu Makubalinao yenu ni yepi tangu mwanzo
 
Habari za wakati huu;
Ni muda mrefu sana sijaweka andiko katika Jukwaa letu hili pendwa ambalo lina wachangiaji wachache.Nikiri tu kwamba ni kwa sababu mbalimbali sijaweza kuweka andiko hapa haswa kutokana na changamoto mbalimbali za kibiashara na kimaisha.Kama ilivy kawaida yangu huwa napenda kujaribu aina mbalimbali ya Biashara na kwa kweli katika kipindi kirefu kilichopita niliingia katika aina tofauti ya Biashara ambayo nitaaita uwekezaji.Ndio nilihama katika kuwa mfanya biashara anayeuza bidhaa na huduma na kuwa mfanya biashara anayeuza na kununua mtaji.Sikuacha baadhi ya shughuli nilizokuwa nafanya na wala sikubadilisha mfumo wangu wa ufanyaji kazi.Lakini nilibadilika na kujaribu bahatri yangu katika uwekezaji.

Kiuhalisia sikuwa na ukwasi(utajiri) mkubwa wa kuweza kuwa mwekezaji mkubwa anayetengeneza Faida hivyo basi kwa kiwango kukubwa nilitumia kamtaji kango kadogo kufanya uwekezaji katika kampuni kwenye soko la hisa la Dar es Salaam na Fedha nyingine niliwekeza katika kampuni za watu binafsi ambao nilifhamiana nao na kwenye kampuni nyingine niliwekeza muda na ujuzi wangu kidogo kwa kiwango kidog cha umiliki katika kampuni hizo.Kwa mchanganuo tu asilimia 40 ya mtaji wangu niliokuwa nao niliwekeza kwenye soko la Hisa na DSE asilimia 60 nyingine iko kwenye kampuni binafsi ambazo haziko kwenye soko la hisa.

Katika kampuni hizi binafsi ambazo mimi nilikuwa kama Sehemu ya wajumbe na Pia kama mshirikia katika baadhi ya shughuli za utendaji nilijifunza kwamba Faida niyokuwa ninapata ilikuwa kubwa kuliko faida niliyokuwa ninapata katika SOKO la hisa.Ingawa kwenye Soko la hisa Usalama wa Pesa yangu nauona uko JUU lakini kwenye kampuni Binafsi niliona usalama wa Pesa yangu ukiwa mdogo hata hivyo faida niliyopata ilikuwa ni nzuri zaidi.Ili kujilinda kuna Mbinu nilitumia ikiwamo kuwa na Debentures kwenye baadhi ya kampuni nilizoweka Pesa zangu hasa zile za Binafsi huku nikiwa ni sehemu ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.Kwa sababu hiyo nilijifunza pia kuhusu aina mbalimbali za biashara ambazo nisingeweza kujifunza mwenyewe.

Hata hivyo katika Kufanya Shughuli hizi nilijifunza mambo mengi sana ambayo mengine niliyafahamu kabla na mengine sikuwahi kuyaona yakifanyika moja kwa moja.Baadhi ya mambo hayo ndio ambayo yamenifanya niandike Uzi Huu:
  1. Kwanza hakuna biashara ambayo hailipi.Biashara zote zinalipa cha muhimu ni utambue wateja wako ni wapi na uwezo wao wa kulipa ni upi.
  2. Pili nilijifunza kwamba Cashflow is Kingi(Yaani Biashara yenye Mzunguko Mkubwa ndio Biashara)Haijalishi una casha kiasi gani,mtaji mkubwa kiasi gani ila kama Pesa yako haizunguki lazima utafute namna ya kuizungusha
  3. Tatu nikajifunza kwamba Mtaji Sio Pesa.Mtaji ni kila ambacho unaweza kupata kwa kutumia Pesa.Hivyo basi Unapofikiria kuhusu Mtaji Fikiria namna ambavyo uanweza kuvipata vile unavyohitaji bila kutumia Pesa ili uounguze mahitaji ya Pesa kwenye Biashara yako.Hii upunguza Pressure kwenye Mzunguko wako wa Pesa
  4. Nne nilijifunza kwamba (Your Network is Your Networth) wekeza katika kutengeneza mtandao wako na watu unaofahamiana nao.Fahamiana na watu wenye Pesa,wenye maarifa,wenye taarifa,wenye fursa na wenye Mtandao mpana.Hakikisha kwamba mtandao wako unakuwa Mkubwa ila usiwe mtandao ambao unakugharimu sana wewe katika kuwa nao.
  5. Tano nilijifunza kwamba Ni lazima mtu yeyote ambaye ana mpango wa kuwa Tajiri na mwenye ukwasi mkubwa awe na Kmapuni ambayo ni LIMITED na awe na TRUST FUND ambayo itahifadhi mali zake ili zisiathiriwe pale mambo yanapoenda mrama.Ni lazima awe na bima kwa kila aina ya majanga yanayoweza kutokea na ni lazima awe tayari kudaiwa na kudai.
  6. Sita nilijifunza kwamba ni muhimu sana kuwa na Benki inayotambulika.Kwani Benki ina uwezo wa kuzalisha Pesa.Ili kumiliki Benki unaweza kuanza na Kumiliki SACCOS.Ndio SACCOS ni Benki na kama unahitaji utajiri ni lazima UMILIKI BENKI maana kupitia BENKI ni rahisi sana KUPATA PESA
  7. Saba niljifunza Pia kuhusu umuhimu wa Kuwa na mfumo wa Soko UNaojitegemea(Closed Market System) Kwa mfano manweza kuwa na kikundi cha watu ambao mnazalisha bidhaa ambazo nyie ndio watumiaje wake)Kwa mfano kua anayezalisha matunda,mwigine nafaka,mwingine,mboga,mwingine nguo,mwingine vitu vingine.Ambao katika huo mfumo wenu hela inazunguka humo ndani tu na inatoka nje tu pale panmapokuwa na ulazima ila kuingia mnaruhusu hela iingie.Kwa mfano kama nyiye ni wanywaji wa Gambe mnakuwa na Pub ambayo inamilikiwa na mmoja wenu.Na yule wa Pub anakuwa ananunua Sehemu ya Jumla inayomilikwa na mmoja wenu an ikiwezekana mmoja wenu awe na kiwanda kabisa cha Gambe ili mhakikishe kwamba Pesa inayotoka kwenye Mtandao wenu ni ndogo zaidi kuliko ile inayoingia(Balance of Trade)
Haya ni baadhi ya madini ambayo nimejifunza kwa muda ambao nimekuwa mbali na ninyi na nilikuwa Jukwaani kwani ni eneo langu la kujidai.Kama unahitaji Mjadala zaidi kuhusu haya niliyoandika hapa usisite kuwasiliana nasi kwa emails:masokotza@gmail.com au masokotz@yahoo.com.

Nawatakieni kila la heri katika mapambano yenu
Post nzuri mkuu

mkuu naomba kujua, je kwa huku Tanzania kuna trust fund ambazo zipo reliable kumanage asset zetu?, nimefatilia na kusoma sana kuhusu trust funds, na jinsi millionaires wa nchi ze wenzetu wanavo zitumia, na kuzi utilize kupata benefit, wengine hata wakifa unakuta waliandika na waliikabidhi trust fund ichukue jukumu la kuendesha biashara zake, je zipo huku Tanzania?
 
Back
Top Bottom