Good Thinking, Comrades.
Bado nafanya Tafiti. Ni Taifa gani limewahi kupiga hatua za kimaendeleo, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni bila watu wake kupenda kujifunza, kusaili na kudadisi ila jitihada zangu zinagonga mwamba. Sipati jibu kwa urahisi na labda, Jibu ni HAKUNA.
Kwanini sisi tunadhani hili linawezekana?, au pengine litaanzia kwetu?. Kwanini tunapenda kujiondoa ufahamu kwa kiasi hiki?. Siyo baba, mama, jamii na Taifa kwa ujumla.
Rafiki yangu (asiyepungukiwa na kumbukumbu) aliwahi kuniambia "Hakuna kazi rahisi kama kuwaongoza watu wasiopenda kusoma, mbaya zaidi hakuna kitu kibaya kama kuongozwa na watu wasiopenda watu wasome".
Ili ubongo uwe na manufaa kwa binadamu ni sharti uendelezwe, unolewe, ufunzwe, ulindwe, ufanyiwe usafi na kadhalika. Na huku kote husaidiwa kwa kusoma vitabu, kutizama na kusikiliza vipindi vya msingi, kusafiri macho na masikio vikiwa wazi na kadhalika. Huu ndiyo uwezo wa pekee alioutupa Mungu.
Ubongo wa binadamu usipofanyiwa hivi, kisilika hufanana na ubongo wa mbuzi ambao kimantiki husibiri kuliwa na binadamu. Ni lazima tuwe RESTLESS, tusaili, tutafiti, tuulize. Ndivyo walivyofanya kina Gallileo, Copernicus, Socrates, Nyerere, Lumumba na orodha inaendelea.
Ni lini uliwahi kumuona Public Figure (Rais, Waziri, Mbunge, Askofu, Padre) Maktaba?, japo kuhimiza tabia ya Usomaji vitabu?. Sina kumbukumbu vizuri, zaidi tu Namuona Mh Zitto, Makamba, Padre Amigu wakihimiza mitandaoni na kuweka List ya vitabu walivyosoma. That's good somehow, how about others?.
Lakini, Je ni wangapi wenye access ya kuingia mitandaoni na kuona idadi ya vitabu walivyovisoma?. Hatuoni kwa wenzetu utofauti ulivyo mkubwa?. Kila mwisho wa mwaka wanaweka List ya vitabu walivyosoma (kwa kusailiwa), huku ni siasa, siasa, siasa!!
Nashauri, Serikali, Wizara husika iliangalie hili kwa jicho la kipekee. Taifa lisilohimiza watu wake wapende kusoma vitabu linajichimbia kaburi na kuzalisha Taifa la watu wa hovyo kwa miaka na siku za usoni.
Baba akisoma vitabu, mama akisoma vitabu na mtoto pia atasoma vitabu.
Asalaam.