SoC04 Huduma za maji safi na salama nchini kwa kutumia mfumo wa usafishaji maji utumiao nishati ya jua

Tanzania Tuitakayo competition threads

Goldenmind

Member
May 22, 2024
10
9
D324-0476-111.jpg - 2024-06-06T055356.053.jpeg

Chanzo: wordvision.org/blog​

Utangulizi
Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali maji za kutosha kama mito, maziwa na vyanzo vya maji chini ya ardhi. Licha ya ukwasi wa rasilimali hizi takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 55 ya wananchi waishio vijijini na asilimia 86 ya wananchi waishio mijini ndio wana uwezo wa kupata vyanzo safi vya maji (UNICEF).
Jamii nyingi zipatikanazo Tanzania hususani vijijini hutegemea vyanzo vya maji visivyo salama. Hali hii hupelekea jamii hizi kukumbwa na maradhi yatokanayo na utumiaji wa maji yasiyo salama na hivo kuhatarisha afya za wananchi.

Moja kati ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals) yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015, ni lengo namba 6 (SDG6) linaloazimia upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira kufikia mwaka 2030. Tanzania kama ilivyo kwa Umoja wa Mataifa inatambua kuwa ni haki ya kila binadamu kupata maji safi na mazingira safi.

Iwapo Tanzania itachukua jitihada za makusudi ndani ya miaka 10 ijayo, itaweza kuwapatia wananchi wake haki yao ya msingi ya kupata maji safi na salama. Moja ya jitihada hizo ni kuwepo kwa mifumo ya kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua ili kuboresha afya na hali ya maisha ya jamii zetu.

African children fetching and drinking contaminated water(1).jpg

Chanzo: Madeblue.org​

Madhara ya matumizi ya maji yasiyo salama
Matumizi ya maji yasiyo salama hupelekea athari kama:

1. Magonjwa kama vile kipindupindu, homa ya matumbo na kuhara. Kwa mujibu wa UNICEF, ugonjwa wa kuhara ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania, ambapo takriban watoto 27,000 hufariki kila mwaka.

2. Maambukizi ya Vimelea: Maji yaliyochafuliwa yanaweza kuwa na vimelea kama vimelea vya kichocho na minyoo ya utumbo.

BR9091-2-1536x1024.jpg

Chanzo: datelinehealthafrica.org​

Mfumo wa kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua ni nini?
Huu ni mfumo unaotumia nishati ya jua kuvuta maji kutoka kwenye vyanzo vilivyopo juu ama chini ya ardhi na kisha kutumia teknolojia mbalimbali kuyasafisha ili yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.

Sehemu zinazounda mfumo
1. Paneli za sola: Paneli hizi hubadili nguvu ya jua kuwa umeme utaotumika kuwasha pampu ya kuvuta maji kwa ajili ya kuchujwa na kusafishwa. Idadi ya paneli hutegemea ukubwa wa mota ya kupampu maji.
2. Betri: Hutumika kutunza umeme wa ziada utaozalishwa kipindi cha jua ili kuwezesha mfumo kutumika kipindi cha mawingu au usiku.
3. Teknolojia za usafishaji maji: Pampu huvuta maji kutoka kwenye chanzo na kuyapeleka upande wa kusafishwa ili yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu. Zipo teknolojia mbalimbali zitumikazo kusafisha maji kama mfumo wa Reverse Osmosis (RO), Uzuiaji wa Ultraviolet (UV), mfumo wa kuchuja zaidi (UF) na vichujio vya kaboni.
4. Sensor na mifumo ya ufatiliaji na upimaji wa ubora wa maji.
5. Usafirishaji wa mfumo: Mara nyingi mfumo wa kusafisha maji huwekwa kwenye trela au magari ili kusafirishwa.

images_77_fotor_202406066306_V1 (1).jpeg

Chanzo: Kapwing​

Jinsi mfumo unavyofanya kazi
1. Uzalishaji wa Umeme
  • Paneli za jua huchukua mwanga wa jua na kuubadilisha kuwa nishati ya umeme.
  • Kiasi cha nishati ya umeme iliozalishwa hutunzwa kwenye betri kwajili ya matumizi wakati wa usiku au kipindi cha mawingu.
2. Uvutwaji wa maji toka ardhini
  • Maji kutoka kwa chanzo (mto, ziwa, bwawa, au kisima) huvutwa kwa pampu zitumiazo umeme uliozalishwa.
  • Maji haya huchujwa ili kuondoa uchafu mkubwa na mchanga kabla ya kupelekwa kwenye mfumo wa usafishaji.
3. Usafishaji
  • Utando wa kuchuja chembechembe ndogo zaidi: Utando huu huondoa chembe ndogo zaidi, bakteria na protozoa kutoka kwenye maji.
  • Mfumo wa Reverse Osmosis (RO): Mfumo wa RO husafisha zaidi maji kwa kuondoa chumvi zilizoyeyushwa, kemikali na vichafuzi vingine. Hii husaidia kuhakikisha maji ni salama kwa kunywa.
  • Uchujaji wa kaboni ulioamilishwa: Huboresha ladha na kuondoa kemikali kama vile klorini na VOC.
  • Uzuiaji wa Ultra Violet (UV): Mwanga wa UV hutumiwa kuua vijidudu vyovyote vilivyosalia na kuhakikisha maji ni salama kabisa kwa matumizi.
4. Uhifadhi na Usambazaji
  • Maji yaliyosafishwa huhifadhiwa kwenye matanki safi tayari kwa kusambazwa.
5. Ufuatiliaji na Matengenezo
  • Sensor hufuatilia ubora wa maji na utendaji wa mfumo.
  • Matengenezo ya mara kwa mara huhakikisha kudumu kwa mfumo na utendaji wa muda mrefu.
6. Usafirishaji: Mfumo unaweza kusafirishwa kwa urahisi hadi maeneo tofauti inapohitajika.

Tuanzie wapi?
Tanzania tukidhamiria ndani ya miaka 10 ijayo, tunaweza kuanza na mifumo michache ya kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua inayohamishika. Mifumo ya usafishaji maji inayohamishika itasaidia kupunguza gharama za kuanzisha mradi wa usafishaji maji kwani tutaanza na mifumo michache yenye uwezo wa kuhudumia maeneo mengi zaidi.
Mbeleni tutaweza kuboresha huduma hizi kwa kuweka mashine za usafishaji maji zitumiazo nishati ya jua katika kila eneo lenye uhitaji.

images (75).jpeg

Chanzo: green.org

images (76).jpeg

Chanzo: Pinterest.com​

Pichani ni mashine zinazohamishika zitumiazo nishati ya jua kusafisha maji.

Faida kwa jamii na Taifa
Mfumo wa usafishaji maji kwa kutumia nishati ya jua una faida kedekede kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Faida hizo ni kama ifuatavyo:
1. Huboresha afya ya jamii kwa kupunguza magonjwa kama kichocho, kipindupindu na homa ya matumbo na hivyo kuwawezesha watanzania kuwa timamu katika kushiriki kukuza uchumi wa nchi.
2. Huwapunguzia wanawake na watoto wa kike taabu ya kwenda umbali mrefu kutafuta maji salama na hivo kuwapa nafasi ya kutekeleza majukumu mengine yenye tija.
3. Huwapatia nafasi watoto wakike kuhudhuria mashuleni kwa kupunguza masaa ya kwenda mbali kutafuta maji safi na salama.
4. Husaidia kutunza mazingira kwa kupunguza ukataji miti ovyo kwaajili ya kuchemsha maji .
5. Hupunguza vifo na gharama za matibabu zitokanazo na magonjwa yasambazwayo kwa njia ya maji.

Hitimisho
Teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua ni suluhisho thabiti na rafiki kwa mazingira kwenye maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika nchi yetu. Teknolojia hii inatoa njia ya kuaminika na endelevu ya kushughulikia masuala ya uhaba wa maji safi na salama. Endapo Tanzania itachukua hatua kuwapatia wananchi wake maji safi na salama, faida mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kielimu zitapatikana.

โ€œNchi zenye afya nzuri ni nchi zenye watu wenye afya nzuri. Afya njema ni msingi wa maendeleo ya kweli kiuchumi na kijamiiโ€ Julius Kambarage Nyerere
 
Chapisho makini sana hili nimejifunza๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘
ingependeza ukaweka gharama pia ya kufungua mradi mmoja ukilinganisha na mifumo iliopo sasa kwa mfano teknolojia za kuchuja maji kama ro, uv na uf ni ghali sana inafanya tusizitumie katika miradi yetu ya maji.
 
Naam mkuu upande wa gharama nimekuacha wazi nikitaraji kama nchi tukidhamiria vijana wetu wabunifu watatengeneza mifumo hii kitachofanyika ni kuimport vifaa, pia kwakua mashine ni mobile tunaweza kuanza na chache maeneo yaliyo jirani yakishare kupunguza gharama.
 
Sijakuelewa njia hizo nani wa kuzitumia au wakuziwezesha wananchi tuzitumie ni sisi wananchi tununue au serikali iwajibike kufanya haya uliyo ya andika ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama Kwa wananchi wetu Kwa kutumia njia zako.

Sijaelewa key point yako njia hizo ni nani wa kuwajibika n hili kwenye ishu hizi
 
Anha, kwenye utangulizi na hitimisho niliweka maneno yanayoitaka Tanzania kuchukua hatua kuwapatia wananchi wake huduma ya maji safi na salama, nikikusudia Serikali ya Tanzania-Wizara ya maji na umwagiliaji, ambayo husimamia sera, kanuni, na maendeleo ya miundombinu inayohusiana na usambazaji wa maji na usafi wa mazingira katika nchi nzima.
 
View attachment 3011293
Chanzo: wordvision.org/blog​

Utangulizi
Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali maji za kutosha kama mito, maziwa na vyanzo vya maji chini ya ardhi. Licha ya ukwasi wa rasilimali hizi takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 55 ya wananchi waishio vijijini na asilimia 86 ya wananchi waishio mijini ndio wana uwezo wa kupata vyanzo safi vya maji (UNICEF).
Jamii nyingi zipatikanazo Tanzania hususani vijijini hutegemea vyanzo vya maji visivyo salama. Hali hii hupelekea jamii hizi kukumbwa na maradhi yatokanayo na utumiaji wa maji yasiyo salama na hivo kuhatarisha afya za wananchi.

Moja kati ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals) yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015, ni lengo namba 6 (SDG6) linaloazimia upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira kufikia mwaka 2030. Tanzania kama ilivyo kwa Umoja wa Mataifa inatambua kuwa ni haki ya kila binadamu kupata maji safi na mazingira safi.

Iwapo Tanzania itachukua jitihada za makusudi ndani ya miaka 10 ijayo, itaweza kuwapatia wananchi wake haki yao ya msingi ya kupata maji safi na salama. Moja ya jitihada hizo ni kuwepo kwa mifumo ya kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua ili kuboresha afya na hali ya maisha ya jamii zetu.

View attachment 3011294
Chanzo: Madeblue.org​

Madhara ya matumizi ya maji yasiyo salama
Matumizi ya maji yasiyo salama hupelekea athari kama:

1. Magonjwa kama vile kipindupindu, homa ya matumbo na kuhara. Kwa mujibu wa UNICEF, ugonjwa wa kuhara ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania, ambapo takriban watoto 27,000 hufariki kila mwaka.

2. Maambukizi ya Vimelea: Maji yaliyochafuliwa yanaweza kuwa na vimelea kama vimelea vya kichocho na minyoo ya utumbo.

View attachment 3011295
Chanzo: datelinehealthafrica.org​

Mfumo wa kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua ni nini?
Huu ni mfumo unaotumia nishati ya jua kuvuta maji kutoka kwenye vyanzo vilivyopo juu ama chini ya ardhi na kisha kutumia teknolojia mbalimbali kuyasafisha ili yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.

Sehemu zinazounda mfumo
1. Paneli za sola: Paneli hizi hubadili nguvu ya jua kuwa umeme utaotumika kuwasha pampu ya kuvuta maji kwa ajili ya kuchujwa na kusafishwa. Idadi ya paneli hutegemea ukubwa wa mota ya kupampu maji.
2. Betri: Hutumika kutunza umeme wa ziada utaozalishwa kipindi cha jua ili kuwezesha mfumo kutumika kipindi cha mawingu au usiku.
3. Teknolojia za usafishaji maji: Pampu huvuta maji kutoka kwenye chanzo na kuyapeleka upande wa kusafishwa ili yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu. Zipo teknolojia mbalimbali zitumikazo kusafisha maji kama mfumo wa Reverse Osmosis (RO), Uzuiaji wa Ultraviolet (UV), mfumo wa kuchuja zaidi (UF) na vichujio vya kaboni.
4. Sensor na mifumo ya ufatiliaji na upimaji wa ubora wa maji.
5. Usafirishaji wa mfumo: Mara nyingi mfumo wa kusafisha maji huwekwa kwenye trela au magari ili kusafirishwa.

View attachment 3011296
Chanzo: Kapwing​

Jinsi mfumo unavyofanya kazi
1. Uzalishaji wa Umeme
  • Paneli za jua huchukua mwanga wa jua na kuubadilisha kuwa nishati ya umeme.
  • Kiasi cha nishati ya umeme iliozalishwa hutunzwa kwenye betri kwajili ya matumizi wakati wa usiku au kipindi cha mawingu.
2. Uvutwaji wa maji toka ardhini
  • Maji kutoka kwa chanzo (mto, ziwa, bwawa, au kisima) huvutwa kwa pampu zitumiazo umeme uliozalishwa.
  • Maji haya huchujwa ili kuondoa uchafu mkubwa na mchanga kabla ya kupelekwa kwenye mfumo wa usafishaji.
3. Usafishaji
  • Utando wa kuchuja chembechembe ndogo zaidi: Utando huu huondoa chembe ndogo zaidi, bakteria na protozoa kutoka kwenye maji.
  • Mfumo wa Reverse Osmosis (RO): Mfumo wa RO husafisha zaidi maji kwa kuondoa chumvi zilizoyeyushwa, kemikali na vichafuzi vingine. Hii husaidia kuhakikisha maji ni salama kwa kunywa.
  • Uchujaji wa kaboni ulioamilishwa: Huboresha ladha na kuondoa kemikali kama vile klorini na VOC.
  • Uzuiaji wa Ultra Violet (UV): Mwanga wa UV hutumiwa kuua vijidudu vyovyote vilivyosalia na kuhakikisha maji ni salama kabisa kwa matumizi.
4. Uhifadhi na Usambazaji
  • Maji yaliyosafishwa huhifadhiwa kwenye matanki safi tayari kwa kusambazwa.
5. Ufuatiliaji na Matengenezo
  • Sensor hufuatilia ubora wa maji na utendaji wa mfumo.
  • Matengenezo ya mara kwa mara huhakikisha kudumu kwa mfumo na utendaji wa muda mrefu.
6. Usafirishaji: Mfumo unaweza kusafirishwa kwa urahisi hadi maeneo tofauti inapohitajika.

Tuanzie wapi?
Tanzania tukidhamiria ndani ya miaka 10 ijayo, tunaweza kuanza na mifumo michache ya kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua inayohamishika. Mifumo ya usafishaji maji inayohamishika itasaidia kupunguza gharama za kuanzisha mradi wa usafishaji maji kwani tutaanza na mifumo michache yenye uwezo wa kuhudumia maeneo mengi zaidi.
Mbeleni tutaweza kuboresha huduma hizi kwa kuweka mashine za usafishaji maji zitumiazo nishati ya jua katika kila eneo lenye uhitaji.

View attachment 3011297
Chanzo: green.org

View attachment 3011298
Chanzo: Pinterest.com​

Pichani ni mashine zinazohamishika zitumiazo nishati ya jua kusafisha maji.

Faida kwa jamii na Taifa
Mfumo wa usafishaji maji kwa kutumia nishati ya jua una faida kedekede kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Faida hizo ni kama ifuatavyo:
1. Huboresha afya ya jamii kwa kupunguza magonjwa kama kichocho, kipindupindu na homa ya matumbo na hivyo kuwawezesha watanzania kuwa timamu katika kushiriki kukuza uchumi wa nchi.
2. Huwapunguzia wanawake na watoto wa kike taabu ya kwenda umbali mrefu kutafuta maji salama na hivo kuwapa nafasi ya kutekeleza majukumu mengine yenye tija.
3. Huwapatia nafasi watoto wakike kuhudhuria mashuleni kwa kupunguza masaa ya kwenda mbali kutafuta maji safi na salama.
4. Husaidia kutunza mazingira kwa kupunguza ukataji miti ovyo kwaajili ya kuchemsha maji .
5. Hupunguza vifo na gharama za matibabu zitokanazo na magonjwa yasambazwayo kwa njia ya maji.

Hitimisho
Teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia nishati ya jua ni suluhisho thabiti na rafiki kwa mazingira kwenye maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika nchi yetu. Teknolojia hii inatoa njia ya kuaminika na endelevu ya kushughulikia masuala ya uhaba wa maji safi na salama. Endapo Tanzania itachukua hatua kuwapatia wananchi wake maji safi na salama, faida mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kielimu zitapatikana.

โ€œNchi zenye afya nzuri ni nchi zenye watu wenye afya nzuri. Afya njema ni msingi wa maendeleo ya kweli kiuchumi na kijamiiโ€ Julius Kambarage Nyerere
Hongera sana.
 
. Safi sana mkuu, haki ya kushinda ulikuwa nayo. ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

. Hongera sana
 
Back
Top Bottom