HUDUMA YA TIGO BIMA

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,351
Habarini wandugu!
Nashukuru kwa wasaa wenu wa kusoma uzi huu...
JE Umeshawahi sikia au tumia Huduma ya tigo bima?

Nimeamua kuuliza hivi kwakuwa nmeshapigiwa simu mara kadhaa na wahudumu wa tigo bima wakijaribu kinishawishi nijiunge kwa kusema kwamba kwa kiasi cha sh. 10000 kwa mwaka basi nitakuwa covered na ajali yeyote itakayotokea kwa ku-nicompasate kwa kiasi cha mil.3.

Kwakuwa Huduma hii siyo mpya na kwakuwa JF ni jukwaa la watu werevu nahisi kunawatu wanaweza toa ushuhuda kuhusu Huduma hii kabla sijafikia kujiunga nayo.

kuuliza kwangu kunatokana na experience yangu mbaya Hasa kwenye Huduma zinazohusu madai.

Naomba mtoe mawazo kuhusu Huduma hii kama ni nzuri au mbaya na kama kuna mtu ameashawahi nufaika nayo au kama kinachochote ambacho kinaweza kutunifaisha wana JF.

Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…