Positive Na Steved Tuongelee Mtu Ambaye Sio Expert Hajui Cmos Ni Nini , Hajui Jumper Ni Nini Huyu Tumsaidieje ?
Zaidi Ya Kumwomba Anunue External Case ?
Pia Umewahi Kureset Bios Ya Compaq Evo Mfano Uone Kinachotokea ??
Shy, Nimekusikia hoja yako...
ILA kilichonipelekea kumuunga mkono PositiveThinker na solution yake hapo juu ni kuwa,
sidhani hata description ya tatizo la computer yake imetolewa kwa marefu, amesema tu kuwa hdd yake ime crush na kuwa kashanunua nyingine, hatujui kama ni mpya au kuukuu..
Watu tuna filosofia mbalimbali katika kutatua matatizo, mimi kwenye matatizo ya computer mara nyingi hutumia mbinu ya elimination... tatizo baada ya tatizo, nikiwa na uhakika na tatizo langu na sababu zake. Hivyo basi ningekuwa mimi mtu wa kwanza kutoa comment hapo juu, wala nisingemwambia kuwa anunue case ya kuweka hdd yake, sijui alichonunua kama kinafaa, kama kime kuwa tested, pia sijui kama anajua jinsi ya kukiunganisha... hivyo kama mtu ambaye anatafuta ushauri, kumtuma tu akanunue kitu kingine mimi sioni kama ni njia nzuri ya kutaka kutatua tatizo ambalo halijaelezwa vizuri na kuwa na uhakika nalo.
Hata hayo maelezo ya PositiveThinker, nisingeenda huko kote kutaka kumuelekeza mtu ambaye kipimo cha ujuzi wake sinauhakika nao. Basi kwa elimination, ningetoa wazo moja baada ya jingine na kuona kitu gani kinafanya kazi na nini hakifanyi kazi, pia sababu za computer kuharibika. Sasa kama hapo juu tunavyotaka kumuelekeza na kujikuta kumbe computer yake ilidondoka na circuit board yake imecrack kiaina hivyo haikamilishi mawasiliano ya ndani kwa ndani, nasi tunamwambia akanunue kitu kingine... fikiri sasa,afanye hivyo halafu akute hata ports za connection pia hazi detect kitu externally... what do you do, go for refund or...Naomba kuishia hapa kuhusu hili. Ahsante.
Shy, kuhusu Compaq, sijatumia sana (sijatengeneza) siku za hivi karibuni, mara ya mwisho ilikuwa 1999, nakukumbuka nilipokuwa nafungua cases za desktop na kujikuta nahitajika kununua security screw driver set kwa ajili ya kufungua cases zake tu...Wanavyofanya firmware lock ya CMOS it's interesting point, nitacheck na kusoma matatizo ya CMOS zake, walau hizo za zamani kama vile Endeleaaa anataja pia. Lakini pia najua some of Dell machines, especially servers nazo zinatumia technique hiyo ya ku-lock CMOS na POST code, ukishatoa hdd yake tu mpaka upate CMOS password kutoka kwao ambazo ziko serialised na hdd. **As a matter of fact, it is quite possible that Buswelu's problem might relate to this***
Baadae.
SteveD.