Wakuu,
Lissu amepiga hotuba moja safi sana, Mbowe karudi kule kule kuanza kuanza kuongelea historia ya chama, mara kusifia wafanyabiashara (wanaompa hela za kuhonga wajumbe ), mara aanze kupiga majungu kuhusu matusi kwenye chama, yaani bure kabisa.
Ndio maana huyu alikimbia mdahalo kama Nchimbi, confidence kubwa lakini content 0, angevuliwa nguo ikawa fezea
======
Mbowe ameanza kuongelea kuhusu kumbukumbu ya CHADEMA kupata usajili wa kudumu Januari 21/1993 wakiwa wanatimiza miaka 32, akisema imekuwa safari ya aina yake iliyojaa mishale na mateso, huku wengi wa wananchama hao wakiwa hawajaweza kufika kuiona siku ya leo.
Mbowe ameendelea kwa kuwatambua wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye mkutano huu ikiwemo wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisahahaulika, ikiwemo Joseph kusaga. Akamwambia muda wowote akijisikia kuamia CHADEMA watamkaribisha kwa mikono miwili.
Asema kwa yeyote atakyeshinda ahakikishe matusi, kubezana na kejeli kwa wengine isiwe utamaduni wa CHADEMA. Asema wanaweza kuvumilia kipindi hiki cha uchaguzi, lakini uchaguzi ukiisha lazima wakasafishe suala hili.
Pia soma: LIVE - Pre GE2025 - Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?
Mbowe asema hawapo CHADEMA sababu ya kujifurahisha tu, bali wako hapo sababu wana malengo ya kutimiza, na malengo haya yatatimizwa na watu wote.
Mbowe asema kuna matatizo mengi nchini na umasikini uliokithiri ambao kama chama cha upinzani wanatakiwa kufanya jambo. Asema akifikiria haya huwa anakosa usingizi. Na ili waweze kutimiza haya inabidi kuwe na uchaguzi wa haki na haki huru, ambako bila mabadiliko kwenye sheria na taratibu za uchaguzi hayataweza kutokea.
Kupata hotuba ya Lissu angalia hapa: Pre GE2025 - Hotuba ya Lissu Uchaguzi Mkuu CHADEMA: Asema amekuwa na Mbowe kwa zaidi ya miaka 20 bila kugombana, amshukuru
Amalizia kwa kuwashukuru wanachama wengine kwa kuongoza chama lakini bado hawajafika wanapotaka, ambako amesema haijalishi wanachama wamekaa miaka mingapi kwenye chama muhimu ni kushirikiana pamoja kuhakikisha wanafikia malengo yao.
Aongeza pia anaamini uchaguzi huu utaisha salama, kusiwe na kiburi kwa yeyote atakayeshinda bali waungane na kusherekea pamoja, na kushirikiana pamoja wakiwa na umoja kusonga mbele.