Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,080
- 67,505
KITOTO CHA AFU MBILI
Mtunzi: Robert Heriel
#+255693322300
Age. 18+
EPISODE 01
"Unafikiria nini Mpenzi"
" Mmmh! Sio Jambo kubwa!"
" Upo mbali Sana. Kama sio Jambo kubwa litakuwa Jambo gani "
" Bado natafakari mtunzi wa simulizi ya mapenzi yetu. Natamani ningemwona anafananaje. Ni mtu wa aina gani! Natamani ningemwona walahi!"
" Hahahaha! Baby unaongea kama unaota. Unafikiri maisha yanamtunzi?"
" Kuna wakati nilijaribu kufikiria kuhusu hilo lakini kila nilipokaribia Kupata jibu kwa kweli nilihisi ninachofikiri hakipo sahihi. Wapo wanaosema mtunzi wa maisha ni Mungu mwenyewe, wengine wanadai maisha yametokea kibahati bahati. Wengine hawajishughulishi na chochote kuhusu mambo hayo. Ni kama haiwahusu Sana"
" Wewe utakuwa unaamini kuhusu maisha yameinjiniwa na Mungu ndiye unamuita Mtunzi?'"
" Sijielewi"
"Hahahaha" wote wanajikuta wanacheka kisha wanachukua glass Zao zenye vinywaji wanakunywa.
" Kuna wakati nahisi maisha yametokea kibahati tuu. Lakini hisia zangu zinanikatalia nikiyaona mahusiano yetu yalivyo. Siamini Kabisa kwamba nyuma ya hizi raha hakuna Mtunzi. Kwamba yametokea kibahati bahati. Hapana Darling!"
" Kwamba nini? Unamaanisha...."
"Mtunzi wa simulizi yetu ni MUNGU " wakaongea kwa pamoja.
Papo hapo kukawa Giza. Giza! Giza! Giza!
*****************
Mimi sio Mungu, Mimi ni mtu kama watu wengine. Isipokuwa Mimi ni Mtunzi niliyewaumba ninyi wahusika kwenye simulizi hii. Kamwe hamtokuja kuniona Mimi Mtunzi wenu niliyewaumba. Ila Mimi ninawajua kwa Sababu ndiye nimewapa Uhusika na majina. Ninampa ninmtakaye na ninamnyima nisiyemtaka.
Sitaki muwaze mambo kama hayo
Mkanigombanisha na Mungu wangu. Sasa nitawaamulia chakufikiri na chakufanya. Nilitaka mjiamulie wenyewe, muwe huru. Lakini nimeghairi. Mnataka kuniona! Ajabu kuu!
***********
Umeme ulikuwa umekatika wakati Vanessa akijivinjari na mpenzi wake.
"oops! this is not right! Umekatikaje wakati nilitaka nishuke chini tukacheza Muziki Casino!"
" Usijali honey! Humu wanajenereta! Vita subira" Kabla huyu mwanaume hajamaliza kuzungumza umeme ukarudi.
"Huoooo!" Wote wakajikuta wakisema kwa pamoja kisha wakanyamaza kwa pamoja.
Alafu Vanessa akaachia cheko la haja lililojaza chumba kizima.
Yule mwanaume wa Makamo akawa akatabasamu tuu.
"Haaah! Umenifurahisha kweli! Ulivyosema huooo! Hahaha! Kumbe Mpaka ninyi watu wazima " Vanessa alizungumza kimahaba lakini Sauti yake akaibadilisha alipomuiga Mwanaume huyo wa Makamo.
"Twende Basi tukacheze muziki."
"Sawa Bebe V. Acha nivae" Yule mwanaume wa Makamo. Akawa anavaa wakati huo Vanessa Akiwa anajipodoa kwenye kioo huku aliseti vizuri Nywele zake aina ya Slay queen ambazo sio tuu zilimpendeza bali pia zilimfanga aonekane kama mwanamke mwenye mvuto zaidi.
" V nafikiri Mimi tayari"
Hapo V akaamka upesi kama katoto akaruka mpaka aliposimama Yule Mwanamke Mwanaume wa Makamo, akasimama mbele yake wakawa wanatazamana. Kisha Vanessa akawa anamtengeneza Kola ya shati na kumuweka Sawa Yule Mwanaume wa Makamo.
Akapiga hatua mbili nyuma kisha akawa anamtazamo Yule mwanaume kuhakikisha amemuweka sawasawa.
" Smartboy! My handsome! Mwaaah! Umependeza!" Vanessa akasema huku Akiwa amemkaribia tena yule mwanaume akambusu mmwaaah!
"Let's go... Time to parrriii...." Akawa anamvuta Mkono.
" No wait!" Yule mwanaume wa Makamo akamzuia
"What....... why "
"Oooh! Daddy don't be shy. Nipo comfortable hivi.." Vanessa alikuwa amevaa tuu kichupi cha kiajabuajabu na kinguo cha juu kilichoacha kitovu wazi huku baadhi ya sehemu za matiti zikiwa matatani. Miguuni alikuwa amevaa kikuku.
Yule Mzee wa Makamo akawa anamtazamo tuu bila kuwa na maamuzi ya Moja kwa Moja.
"please Honey! Let me do it for my happyness!"
Yule Mzee wa Makamo hakuwa na njia zaidi ya kumkubalia.
Yule Mzee wa Makamo akafungua kwenye Kabati lililokuwa Mule ndani. Ambalo lilikuwa limenakshiwa kwa ufundi wa Hali ya juu. Kuna sehemu Katika Ile Kabati iliandikwa Casino tools. Chini yake kulikuwa na sehemu ya kushika ili uvute. Yule mwanaume akafungua kwenye Casino tools. Hapo akapokelewa na vifaa vya kike na vya kiume vinavyotumika kwenye Casino la Ile Hotel.
Akachambua chambua akatoa barakoa mbili zinazoziba Uso wote kasoro sehemu ya macho palikuwa pamewekwa kioo cha rangi ya Bluu na Ile barakoa nyingine kioo cha rangi ya pinki kumuwezesha mvaaji kuona.
Vanessa akachukua Ile barakao yenye vioo vya pinki na Yule mwanaume wa Makamo akachukua barakoa yenye vioo vya bluu machoni. Wakavaa usoni kila Mmoja kisha wakatoka mule chumba kuelekea kwenye Casino.
****************
COLOMBO HOTEL!
Nje ya Hotel, Upande wa chini ilikuwa imepaki Toyota IST ya kijivu ikiwa na vioo vya tinted. Ndani yake alikuwepo James pamoja na mwanamke Mmoja wa Makamo. Ndani ya gari hiyo kulikuwa na mjadala ulikuwa ukiendelea.
" Hapa ukienda hivihivi hawawezi kuturuhusu, watahitaji ID zetu Halisi Jambo ambalo Mimi sipo tayari kutoa ID yangu"
" Kwa sababu gani hutaki?"
" Sitaki ijulikane nilikuwa humu. Ni Hatari Sana James"
"Okay! Kwa hiyo Mpango wako ni upi?"
" Itatubidi tufanya hivi. Utanisamehe!"
"Sijakuelewa!"
" Tunaenda pale tukiwa kama wapenzi"
" Haaa! Alafu" James akawa anamtazama Yule Mama wa Makamo kwa mshangao huku akimkagua na kulinganisha umri alionao na mwonekano wake kama unaendana na yeye.
" Tutawahonga wale walinzi kisha watatupa passcode ya kuingia. Sijui wanatumia Kadi au kitu gani tutajulia pale"
" Vipi wakitukatalia?"
"Hahaha! James bhana!" Akaendelea
" Uliona wapi mtu akakataa pesa? Kilichowaweka pale ni Pesa. Kila mtu anatafuta pesa. Wengine wanahatarisha maisha yao kisa Kupata pesa sembuse pesa hii ilitojileta mwenyewe. Embu Twende!"
Gari ikatiwa Moto. Wakaingia kwenye Ile Hotel. Pale getini, James ndiye akatoa kitambulisho chake kwa Sababu ndiye alikuwa dereva. Kisha wakaruhusiwa kuingia ndani.
Wakatoka ndani ya gari na Moja kwa Moja wakaelekea kwenye lango la kuingilia lililokuwa linamwekua mwekua likiwa na maandishi yenye taa za kijani yaliyosomeka Colombo Casino. Nje ya lango lile walikuwepo wanaume vijeba wawili waliovalia Suti nyeusi, Miwani nyeusi na Mikono yao ikiwa na glovu nyeupe.
Walipofika pasipo salama kijeba Mmoja akawafuata kama hatua Moja hivi kisha akanyosha Mkono akidai kupewa kitu Fulani.
Alipoona hawaelewi akasema "Passcard"
Hapohapo yule mwanamke wa Makamo akaingiza Mkono kwenye Mkoba wake akatoa Noti za Dola miamia kama Noti kumi hivi. Akamnyooshea Yule kijeba.
Yule kijeba akawatazama, kisha akazitazama zile pesa. Alafu akamgeukia Mlinzi mwenzake. Wakapeana ishara. Yule kijeba akawageukia tena, akazipokea zile pesa. Akazihesabu. Zilikuwa Noti kumi za Dola miamia.
Akawauliza, mnataka nini.
Yule Mwanamke wa Makamo anajibu,
" Tunataka kwenda kujirusha. Huyu Kijana nataka akanifurahishe"
" Sawa!"
Yule kijeba akarudi kwa mwenzake kisha mwenzake naye akazihesabu, natazama wakagwana Noti tanotano alafu Mmoja wa wale vijeba akaingia ndani.
Baada ya dakika kama tano hivi akarudi Akiwa na Kadi pamoja na Barakoa. Akawapa.
Wale vijeba wakanong'onezana Jambo Fulani kisha Yule kijeba aliyepokea zile pesa akawaamrisha wamfute.
Lango likafunguliwa wakaingia ndani
Macho ya James Muda wote yalikuwa juujuu yakishangaa fahari ya mandhari ya mule ndani. Kila alichokiona kwake kilikuwa na sifa ya kipekee. Wakaingia kwenye Lifti. Wakabonyeza kitu cha kuwapeleka ghorofa ya Tatu iliyokuwa underground.
Haikufika dakika Moja wakawa wamefika. Wakatoka kwenye Ile Lifti. Mbele Yao walikuwa wanakabiliwa na mlango mwingine. Yule kijeba akabonyeza bonyeza namba Fulani ule mlango ukafunguka. Hapo wakapokelewa na harufu nzuri mbele Yao kukiwa na korido tatu. Wakachukua korido iliyokuwa mbele Yao ambayo mbele kabisa kulikuwa na lango lililoandikwa Colombo Casino. Wakasonga Mpaka kulikabili.
Kijeba akawaonyesha jinsi ya kutumia zile Kadi ili kufungua ule Mlango.
Pembeni ya ule Mlango kulikuwa na alama za maelekezo kwa kifupi uwapo Colombo Casino. Moja ya maelekezo ni kuvaa Ile barakoa ya Uso. Na kukiuka Sheria hiyo adhabu Kali ingetolewa.
Hapohapo wakavaa barakoa usoni.
Kisha wakaweka Kadi kwenye Mlango, ukafunguka kisha wakaingia ndani!.
************
James alikuwa macho juu akijaribu kushangaa maajabu ya fedha yaliyokuwa mule ndani. Ni kweli mandhari ya Colombo Casino yalikuwa ya kifahari, yakuvutia na yenye kutamanisha lakini anasa zilizokuwa zinaendelea humo zilikuwa anasa za kishetani. Wala usingedhani kuna binadamu wanafanya mambo Yale.
James hakusahau kilichompeleka Mule ndani. Alitaka kumwona huyo mwanaume anayetaka kumnyang'anya Mrembo wake, ndiye Vanessa. Taarifa alizopewa kuwa Vanessa mpenzi wake anatoka na mwanaume mwingine sio tuu zilimuumiza moyo wake lakini pia zilimfanya apate ugeni WA kisasi cha ajabu huku moyoni mwake alidhamiria kuwa atakapokutana na huyo mwanaume ataitoa Roho yake.
Baadhi ya kumbukumbu za hapa na pale za walivyokuwa pamoja na Vanessa zilikuwa zikipita mara kwa mara akilini mwake na hii ndio ilimfanya azidi kupandwa na hasira ya kuua Mtu.
MAzingira ya mule ndani hayakuwa rafiki Sana, asingeweza kumwona Vanessa kwa sababu nusu ya wanawake mule ndani walikuwa wapo uchi wa mnyama. Robo Yao walikuwa wamevaa vichupi huku matiti Yao yakiwa yako matatani. Wachache Sana walikuwa wamevaa nguo za kuzugia. Wote usoni sura Zao zilikuwa zimefichwa na barakoa.
James kila alipojitahidi kumtafuta Vanessa hakuweza kumwona. Jambo jingine kumwekua mwekua kwa zile taa za Casino pia kuliongeza kazi kubwa ya kumpata Vanessa.
Wakati James akihangaika Kwa namna yake, Yule Mwanamke wa Makamo yeye alishakwisha kuwaona Vanessa na Yule Mwanaume Muda mrefu sana. Kitu pekee kilichomfanya awaone kwa haraka ni Ile suti aliyoivaa Yule Mwanaume wa Makamo. Ni suti hiyohiyo ambayo asubuhi Yule Mwanamke wa Makamo aliinyoosha kwa Pasi.
Yule Mwanamke Muda wote alikuwa na hasira Kali juu ya Vanessa. Moyoni alidhamiria siku atakayomkamata Vanessa Basi angemuua. Licha ya kuwa alishakubaliana na James kuwa asije akamdhuru Vanessa.
Kumbe kila Mmoja nafsini mwake aliapa kumfanyia unyambisi mgoni wake.
Yule Mwanamke wa Makamo, akanyanyuka,
"Unaenda wapi?" James akaongea kwa ishara.
" Subiri hapa. Naenda Msalani maramoja" Yule Mwanamke wa Makamo naye akamjibu kwa ishara
James akaachwa hapo.
Lakini James hakuwa mjinga, alikuwa akimfutilia kwa macho Yule Mwanamke wa Makamo alipokuwa akienda. Y
Akashangaa kumwona Yule Mwanamke akichukua uelekeo usio wa Msalani. Jambo ambalo lilivuta umakini wake.
Natazama akamwona Yule Mwanamke akimgusa mwanaume Mmoja ambaye amevaa barakoa. Akawaona wakitazamana pasipo kusema chochote. Yule mwanaume wa Makamo hakumtambua Yule Mwanamke wa Makamo. Vanessa kuona hivyo akamsukuma Yule Mwanamke wa Makamo akaanguka chini Jambo ambalo likazua taharuki kwenye Casino.
Kwa upesi James akawafuata, alipofika akamkuta Yule Mwanamke wa Makamo Akiwa pale chini analia.
Akamuinamia Mpaka pale chini kisha akamuinua, Vanessa alikuwa akitukana lakini matusi na Sauti yake haikufua dafu kutokana na kelele za muziki wa Casino.
James akavua barakoa yake akijaribu kumbembeleza Yule Mwanamke wa Makamo. Wakati huo Yule mwanaume wa Makamo bado alikuwa ameshangazwa na tukio lile. Bado alikuwa kashikwa na bumbuwazi.
Vanessa alishtuka alipoona Sura ya James eneo lile. Zaidi ya yote alishangazwa kuona James akimbembeleza Yule Mwanamke.
Itaendelea.......
Kazi zilizopo tayari
1. Kaburi la mwanamuziki
2. Wakala wa Siri
3. Mlango wa 77