DOKEZO Hospitali ya Bugando, Mwanza ina huduma mbovu sana kwa wagonjwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

shilatu

Member
Apr 18, 2015
58
30
Ndugu zangu, kama umewahi kupeleka mtu yeyote mgonjwa utaniambia hiki nilichoona mimi ni sawa ama si sawa. Nilisindikiza rafiki yangu mwaka Juzi aliuguliwa mtoto mgongo wazi kufika pale ikawa huduma mbovu huduma hadi umpatie rushwa daktari ndio ahudumiwe, bahati mbaya sana mtoto akafariki tukazika.

Mwaka jana tukapeleka baba yangu mdogo alishindwa kupumua vizuri kufika huduma zikawa mbovu manesi wanakupita hakuna huduma, yule mzee akafariki.

Mwaka huu tena rafiki yangu kapewa referral kwenda pale nikamwambia usipeleke Bugando mtoto maana huduma zao ni mbovu, akasema anaamini Bugando, tumezika mwezi ulioisha.

Bugando wana huduma mbovu sana. Pia kuna rushwa na kujuana.
 
Bugando wako vizuri sana, nimekaa hapo wiki mbili kumuuguza mdogo wangu wako vizuri sana, nawapa hongera madaktari na manesi. Mungu awabariki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bugando wana huduma bora sana katika hospitali ninazozifahamu.

Hospitali ambayo inaitwa lango la kuzimu ni Mloganzila, ukienda pale una asilimia 85 ya kuwa mzimu
 
. Unavyo enda hospital usitegemee kupona..

. Kama siku yako imefika ni imefika tu, hata ufanyaje huwezi kupona.
 
Kwa sisi tunaoishi pori tukipeleka wagonjwa wetu pale huwa hawarudi

Gharama kubwa za matibabu afu mnarudi na maiti
 
Ndugu zangu, kama umewahi kupeleka mtu yeyote mgonjwa utaniambia hiki nilichoona mimi ni sawa ama si sawa. Nilisindikiza rafiki yangu mwaka Juzi aliuguliwa mtoto mgongo wazi kufika pale ikawa huduma mbovu huduma hadi umpatie rushwa daktari ndio ahudumiwe, bahati mbaya sana mtoto akafariki tukazika.

Mwaka jana tukapeleka baba yangu mdogo alishindwa kupumua vizuri kufika huduma zikawa mbovu manesi wanakupita hakuna huduma, yule mzee akafariki.

Mwaka huu tena rafiki yangu kapewa referral kwenda pale nikamwambia usipeleke Bugando mtoto maana huduma zao ni mbovu, akasema anaamini Bugando, tumezika mwezi ulioisha.

Bugando wana huduma mbovu sana. Pia kuna rushwa na kujuana.
Unasema huduma mbovu ila husemi ni mbovu kvp
Unamaanisha mgonjwa aliekuwa anashindwa kupumua hakupewa oxygen au vp au mlikuwa mnategemea afanyiwe kitu gan na akafanyiwa kitu kipi?
Na huyo mtoto mlitaka afanyiwe nn ambacho hakufanyiwa
 
Back
Top Bottom