MDAU TZ
Member
- Jun 9, 2023
- 12
- 53
Fununu hizo zinaeleza kuwa Taarifa zimetokana na mkutano uliofanyika na mtendendaji mkuu wa Taasisi hiyo nchini, kupitia mtandaoni na kuhudhuliwa na baadhi ya wafanyakazi.
Mtendendaji huyo amesema kwamba kutokana na changamoto za kiuendeshaji, Taasisi inalazimika kufunga baadhi ya vituo na kupunguza Wafanyakazi.
Hata hivyo, kwa mujibu ya mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo akizunguumza kwa faragha na Mdau Tanzania, amekili kuwa Taarifa hizo ni za kweli na zoezi la kufunga vituo hivyo limeshaanza na mwisho wa uendeshaji wake inatarajiwa ni mwishoni mwa wiki hii ambapo itakuwa Tarehe 15/8/2024.
Mtoa Taarifa huyo amesema kwamba tayari baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi katika vituo vinavyofungwa na wale wanaopunguzwa kutoka kwenye vituo vinavyosalia wameshapewa barua za mualiko wa majadiliano ya kuachishwa kazi.
MY TAKE
Katika hili waajiri wengi wanatumia udhaifu wa Sheria ya Kazi inayotumiKa nchini katika kuwachisha kazi wafanyakazi wao pindi tu Taasisi inapopitia changamoto kidogo.
Sheria imempa wigo Mpana mwajili wa kufanya maamuzi bila ya kujali hali ya mwajiliwa.
Pia kutokana na urahisi waliopewa katika kipengele cha kupunguza wafanyakazi hasa kwa sababu za kiuendeshaji.
Ni wakati wa mamlala hisika kufikiria kufanya mabadiliko ya sheria hii ili kuwapa ulinzi na uhakika wa ajira kwa wafanyakazi.