Hongereni wote ambao hamtegemei Mshahara

KISS 100

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
528
1,113
Salamu. Maisha yana shughuli za kujiajiri na kuajiriwa. Kuajiriwa kunakufanya uwe asilimia kubwa mtu wa kulilia month Salary.

Najiuliza hivi wapo watu hawana Kazi yoyote hata ya kujiajiri ila wanafamilia, wanakula, wanavaa, wanasimu na furaha tale.

Mimi nafanya kazi lakini inflation inatuandama na wengi wafanyakazi hatuna furaha.

Hatuna furaha mana unategemea serikali ikufurahishe. Mfumuko wa being ni hatari.

Pongezi nyingi kwa msio na pa kushika na mnaishi. Mnaishije ndugu kama Nina kamshahara ila maisha ni tight sana.
 
Mtu aliyeajiriwa ni sawa na kuku wa kizungu aliyepo bandani, akingojea aletewe malisho; na aliyejiajiri ni sawa na kuku wa kienyeji anayejitafutia malisho mwenyewe.

Jiulize swali, Je kuku wa kizungu akitolewa bandani atakuwa na uwezo sawa wa kujitafutia malisho kama kuku wa kienyeji?​
 
Mimi nilianza maisha kwa kuajiriwa mda mrefu mpaka mda huu, kwa sasa nipo rikizo nikasema nijaribu biashara.

Nilicho gundua biashara ni ngumu sana, kila siku nashindwa kuiona faida yake ni biashara ni ngumu sana.

Ina hitaji mda kujifunza changamoto zake na namna ya kulijua soko na aina ya mahitaji ya wateja wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom