MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,801
Siku hizi usije ukategemea tena ukiwa Hospitali ya Muhimbili ukasikia neno Mochwari ( Mortuary )
Baada ya Kugundua kuwa Kisaikolojia Watu wengi wanaoenda hapo neno Mochwari linawatisha sasa Muhimbili Hospital nao wamejiongeza.
Ni kwamba kuanzia sasa ukiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuulizia Mgonjwa wako yuko wapi ukisikia unaambiwa yupo Wodi ( Ward ) namba 26 basi jua ameshaanza Maisha yake mapya katika Friji za Mochwari ( nikimaanisha kuwa ameshafariki dunia )
Sababu kubwa ya Kubadiki kutoka kupaita Mochwari na sasa Kuitwa Wodi namba 26 ni kwamba kumbe Kitaaluma ( Professionally ) Mtu akifa Kitabibu bado anahesabika ni Mgonjwa mpaka akizikwa hivyo akifa Wodini kwa Wagonjwa na kupelekea Mochwari kule nako japo amekufa lakini huwa anatibiwa na kuhudumiwa vizuri tu kabla Ndugu zake hawajaenda Kumchukua.
Sasa Wewe Siku moja Kurupuka uende zako Muhimbili Hospital na ukiona Kibao cha Wodi namba 26 jipendekeze Kuingia humo ( huko ) ili ukutane na Maajabu na Vitu vya Kutisha na ukawasimulie wa Kukurupuka Wenzako huko Mtaani Kwenu.