Hongereni 107.7 Upendo fm Radio kwa kujitenga na Waongo

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,877
4,476
Tuwapongeze upendo Radio kwa kusimamia maadili ya Vyombo vya habari

Radio nyingine zote sasa zimekuwa ni Kamari,Kamari hata ile ya taifa ni kuhamasiha Kamari tu, matangazo ya waganga wa Kienyeji, Manambii ambao mienendo na matendo yao yanatiliwa shaka, shuhuda za Uongo kuna Radio moja kila ibada wanakamata Malkia aliyetoka kuzimu na anakuwa ni Kiongozi wa Masheatni au wa chama cha kichawi Full utapeli

Lakini Upendo Radio huwezi kusikia watumishi wa Karibu kanisani, sijui natabairi, ssijui shuhuda za kutapika panya wala mahubiri yenye utata.

Wamesimam kweli nakumbuka kuna nabii mmoja alitaka auziwe masaa ya usiku kwa ajili ya mikesha na akatoa mpunga mrefu sana wakamwambia atafanya recorded na mahubiri yake yata editiwa na Wahariri wa UPENDO MEDIA yule tapeli akagoma.

Japo hawana watangazaji wabunifu sana ila vipindi vyao unaweza kusikiliza mtu wa Aina yeyote na umri wowote.

Vipindi vyao vingi ni vya kijamii ila vinaendeshwa kizee sana yani hata Jingle zao hazinibariki sana hazina ubunifu.

Talanta africha show ya John Pazia kidogo iko vizuri

NAWASHAURI KKKT WAIBADILI AU WAONGEZE WATANGAZAJI WABUNIFU HASA KIPINDI CHA HALI HALISI ASUBUHI, NA MICHEZO JIONI

Ni hayo tu 107.7UPENDO FM RADIO, NDIO CHAGUO LAKO POPOTE UENDAPO

UPENDO FM RADIO AMANI KWA WOTE
 
Huwa wanasema hata mbuyu ulianza kama mchicha, Redio ya kidini kutanganza habari za mipira nao ni mwanzo mzuri wa kutangaza kamari, kwahiyo hakuna cha kushangilia hapo.
ni sawa na redio ya kiislamu icheze nyimbo za singeli na bongo fleva ila iache kutangaza kamari halafu ufurahie na kuipongeza.
 
Hapana walianza zamani sana kipindi cha michezo, mbona hawauzi air time kwa manabii wala waganga kama ilivyo wapo radio,praise power na nyinginezo za dini yaan wao wamejitenga kabisa na hao watu
 
Sikiliza tzgospel radio japo ipo online tu habari tunajiunga na radio washirika kama bbc swahili,dw swahili na clouds na tbc semina kutoka kwa mwl Christopher mwakasege live hapahapa tzgospel radio -upako wa burudani Tzgospel Radio
 
Wakati mwingine hivi viredio vya fm vinaokoteza watangazaji wasiokuwa mahiri kitaaluma kutokana na uwezo wao wa kulipa mishahara mizuri. Kuhusu kutumiwa na matapeli na kamari, hiyo redio ni ya kkkt ambako kimsingi inarusha mambo ya imani yao tu na ya kitaifa. Kuna redio moja ya dhehebu fulani nayo imefuata mkumbo wa kuwa na kamari katika vipindi vyake. Kwenye shuhuda za kutapika panya, mijusi, tandu huo ni uongo haiwezekani kitu kitapikwe kikiwa na umbo lake hivyohivyo bila kusagika wala kidogo. Ni wapuuzi wachache wanaoweza kuamini shuhuda hizo feki. Wale wengine wa ulimwengu mzima redio zao wameamua warushe mambo yao tu, hata nyimbo ni zao tu japo wanarusha na mambo ya kitaifa
 
Kabisa Mkuu umesema vyema. Ila Kwa kusimamia tu hayo machache tuwapongeze
 
Hata ile tv yao isiruhusu kutoa airtime kwa matapeli hata kama kama watapewa fedha nyingi. Kuna matapeli wana tv zao na bado wananunua vipindi kwa tv zingine. Zaidi upendo media wawe wanarusha pia mahubiri ya wengine yasiyo ya kitapeli na waweke nyimbo nzuri hata kama si za dhehebu lao. Wanahabari wao watoke wakarekodi mahubiri ya makanisa mengine watajipatia watazamaji na wasikilizaji wengi. Wavunje ubaguzi wa kimadhehebu waende mpaka kwa wapentekoste kurekodi vipindi. Hiyo redio na tv yao itakuwa maarufu zaidi kwa jamii ya wakristo wote
 
Radio Maria Wana frequency Kila sehemu tatizo zao kurudiarudia vipindi
Pia hawana maktaba nzuri ya nyimbo za kikatoliki Kila siku nyimbo n zilezile tena hii miputiti.
 
Radio nyingine zote sasa zimekuwa ni Kamari,Kamari hata ile ya taifa ni kuhamasiha Kamari tu, matangazo ya waganga wa Kienyeji, Manambii ambao mienendo na matendo yao yanatiliwa shaka, shuhuda za Uongo kuna Radio moja kila ibada wanakamata Malkia aliyetoka kuzimu na anakuwa ni Kiongozi wa Masheatni au wa chama cha kichawi Full utapeli
Ni moja ya sababu inayonifanya nishindwe kabisa kusikiliza Radio, ( kutazama Vipindi vya TV ) vya hapa Nyumbani, TZ.

Ni tatizo kubwa kwa kweli.
 
Imekuwa tatizo kubwa sana, kila saa ni kuhamaisha kamari tu na dawa za kuongeza nguvu za kiume
 
Radio Maria Wana frequency Kila sehemu tatizo zao kurudiarudia vipindi
Pia hawana maktaba nzuri ya nyimbo za kikatoliki Kila siku nyimbo n zilezile tena hii miputiti.
kati ya radio zinazonichosha kusikiliza ni radio maria kuna kipindi chao kinaanza usiku saa tatu ni kuomba hela tuuuuuu radio ina zaiid ya miaka kumi hadi sasa inategemea kuchangiwa na waumini. Matangazo ya shule za kanisa tu yanaweza kuiendesha hiyo radio Kwa mwaka mzima
 
Hata ile tv yao isiruhusu kutoa airtime kwa matapeli hata kama kama watapewa fedha nyingi. Kuna matapeli wana tv zao na bado wananunua vipindi kwa tv zingine. Zaidi upendo media wawe wanarusha pia mahubiri ya wengine yasiyo ya kitapeli na waweke nyimbo nzuri hata kama si za dhehebu lao. Wanahabari wao watoke wakarekodi mahubiri ya makanisa mengine watajipatia watazamaji na wasikilizaji wengi. Wavunje ubaguzi wa kimadhehebu waende mpaka kwa wapentekoste kurekodi vipindi. Hiyo redio na tv yao itakuwa maarufu zaidi kwa jamii ya wakristo wote
kweli kabisa. kuna Mchungaji mmoja wa pentekoste nafikiri anaitwa Raphaeli kutoka kiluvya sijui kibamba naye anahubiri pale, nafikiri wakifanyia ushauri huu kazi itakuwa yente
 
Back
Top Bottom