Hongera Sana Tundu Lissu kwa Ushindi Wako—Lakini Changamoto Zinaanza
- Timu yako ilitumia mbinu ngumu na zenye madhara kwa demokrasia nchini, hasa dhidi ya mlezi na kiongozi wenu ndani ya chama, Freeman Mbowe.
- Kejeli na dharau alizofanyiwa Mbowe kupitia Lema zimewapa ushindi wa muda mfupi, lakini zitakuja na maumivu ya muda mrefu katika uongozi wako. Mfano hai ni jinsi Lema alivyochapisha kitabu chake na kukiita "Udhalimu wa Mbowe ndani ya Chadema," kisha akakiweka wazi kwenye ukurasa wake wa X.
- Uliahidi siasa mpya na kujaribu kumchora Mbowe kama mtu aliyeshindwa—ukidai hana mvuto, hakubaliki, na anatumika na serikali. Sasa, dalili zinaanza kujitokeza. Juzi, baada ya Mnyika kuzuiliwa kufanya mkutano na waandishi wa habari, wengi walitegemea vijana wa BAVICHA wasimame imara tofauti na "ulegelege" uliolaumiwa kwa Mbowe. Lakini cha kushangaza, Lema naye analalamika kwenye X, na watu wanamuuliza: "Mbona kama ya Mbowe? Lissu yuko wapi?"
- Kukosa uvumilivu ndani ya timu yako kumeanza kujionyesha mapema. Mdude ameanza kulalamika kwamba kila mara viongozi wa Chadema wanapokosoa CCM kwenye X, wanajibiwa na maswali: "Kwani utawala wa Mbowe ulikuwa wa asali? Si mlichosema utawala wa simba umekuja na shubiri? Bado mnalalamika kwenye mitandao?"