Hongera sana Elizabeth Michael "Lulu"

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
15,236
21,225
Tangu afariki Marehemu Kanumba industry ya filamu imeshuka Sana lakini Leo hii nimebahatika kuona filamu ya Lulu Michael au Elizabeth Michael kupitia YouTube. Movie hiyo inaitwa "Ni noma" Ni kazi nzuri Sana Cha kwanza nilichopenda hakukuwa na ile tabia ya msanii mmoja kuwa kwenye maeneo mengi unakuta producer yeye, director yeye n.k ndio maana kazi imesaidia kuwa nzuri.

Jambo la pili lililo nivutia ni maudhui ya filamu kiujumla amejitahidi kwenda kwenye idea tofauti na movie nyingi za bongo movie maudhui inamuhusu mwanamke ambaye anaishi maisha ya ukanjanja ana foji veti ili apate kazi ikiwa Hana elimu hiyo na mwanamke huyo amecheza Lulu je swali anawezaje kumudu kazi ikiwa Hana elimu hiyo?ukiicheki utapata jibu

Vitu vilivyonivutia ni usheshi ambao upo serious kwenye hii filamu pia quality ya video ipo vizuri.

Washiriki wote waliocheza hii filamu wameitendea haki kabisa, wamevaa vizuri uhusika ikiwemo dude, isarito n.k

NB: Ikiwa mtatoa kazi nzuri Kama hii itasaidia kupandisha soko lenu la filamu.
 
Hiyo ni noma ndio ile Lulu anawapigia pigia madanga simu pale mwanzon? Kama ndio hii sikufika hata kati ila imeanza poa sana...amecheza sana ule uhusika
 
Hivi kwenye movie ,,,bado mtu akiwaza jambo lazima aangalie juu?aisee...! Wanaoangalia bongo movie wana roho ngumu sana..tatizo bongo movie inaanza vizuri lakini mwisho wanamaliza vibaya sana....bado directors sio wabunifu...na hata story unaweza kujuwa itaishaje bila hata movie kuimaliza..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom