Prof Ndalichako ametoa maamuzi ya kufuta utoaji wa matokeo kwa mfumo wa GPS. Watu wamemuunga mkono na kushangilia. Wengi wanasema ni hatua nzuri ya kuitoa elimu yetu "ICU". Mimi pia nampongeza. Mosi kwa kuonyesha tafsiri hasa ya maana ya uongozi kwa kutoa uongozi. Pili kwa kufanya maamuzi yasiyoongozwa na hisia.
Pamoja na hayo ni vizuri tukatambua kuwa "ELIMU" ni Mali ya jamii/Taifa na si serikali. Si jambo jema kuigeuza elimu kama "patching bag" kwa kila mtendaji kufanya anachotaka pindi anapopewa dhamana ya kuongoza. Asasi za kiraia, taasisi za dini na Serikali, taasisi za elimu, wazazi, wanafunzi na wataalam walikatae jambo hili. Wadau niliowataja watambue haki yao waliyonayo ya kushiriki na kutoa maana juu ya mabaliko yoyote katika sekta ya elimu. Prof Ndalichako aandae mfumo utakaozuia elimu kuchezewa kama "patching bag".