Kweli kabisa mkuu! Huu uteuzi aliofanya Magufuli leo nimependezwa nao mno! Kateua watu wanaojikita kwenye majukumu yao na nampongeza sana! Dr. Mgwatu alikuwa anajua sana umuhimu wa ile workshop ya TAZARA!Kwa uteuzi huu anaofanya magufuli, wasomi tushindwe wenyewe, amefanya sasa taaluma zionekane zina thamani mbele ya jamii. Mkwere aliendekeza uswahiba sana kwenye mambo ya kitaaluma matokeo yake siasa ikaingia kila sehemu/sector nchini. Sasa awamu hii wasomi wetu wakishindwa kututoa tulipo hata kimawazo nitakua wa kwanza kupinga umuhimu wa elimu. Awamu hii inajali wasomi zaidi kuliko wanasiasa. Namjua sana Dr. wangu huyu na nna uhakika sio wa chama chenye dola.
Tutahamia wote mkuuAwamu hii wasomi hawa wakituangusha nahamia mombasa nikaanzishe kiwanda cha chumvi sasa!
Na nilishaamua sitaki mrengo wa chama chochote huu ni mwaka wa tatu..nimechoshwa na disapointimenti na eksichuzes nyingi za wasomi.wetu kila wakati sasa naangalia mambo tu kwa kando kama non participant observer kwenye utafiti maana hamna namna.Tutahamia wote mkuu
Mkuu historia inatubana sana, tatizo wanasiasa ndo waliopigania uhuru, wakaweka mifumo na sheria kuhakikisha wanawatawala hadi wasomi na ndo mana sifa ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika tu, na waziri lazima awe mbunge, na waziri ndo wanasimamia utendaji wa wasomi wote.Na nilishaamua sitaki mrengo wa chama chochote huu ni mwaka wa tatu..nimechoshwa na disapointimenti na eksichuzes nyingi za wasomi.wetu kila wakati sasa naangalia mambo tu kwa kando kama non participant observer kwenye utafiti maana hamna namna.
Mrejesho upo wapi baada ya miaka takriban minne ya utumishi? Ingependeza sana kama kusudio la kuifufua mada hii lingekuwa hilo.Naomba kwa dhati kabisa nimpongeze mwalimu wangu na rafiki yangu Dr. Musa Mgwatu, mwalimu asiye na makuu!