Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,961
- 47,828
Kilichotokea kwa Mpina Bungeni, ni kile kilichotarajiwa. Na wala hakuna anayeyashangaa maamuzi ya Bunge, zao la uovu wa 2020.
Bunge ambalo nalo ni matunda uovu na uchafu wa mwaka 2020, limeendelea kudumu katika kanuni ya upatikanaji wake. Ni Bunge la waovu:
1) Mahakama kuu ilitoa hukumu kuwa wabunge wanaoitwa wa kupita bila kupingwa, ni wabunge batili. Na hao ndio waliojaa humo Bungeni.
2) Hili Bunge ndiyo lililoidhinisha ile IGA ya hovyo kabisa iliyopokonya mamlaka ya nchi juu ya rasilimali zake. Kama nchi tunazuiwa na IGA kumtafuta mwekezaji mwingine kwenye masuala ya bandari iwe kwenye mito, maziwa au bahari, mpaka tumtaarifu DPW, na yeye aridhie. Hili ni bunge lililopofushwa na malipo ya DP World. Mbunge aliyekuwa nje ya inner circle anasema walipelekwa Dubai, na wakiwa huko walikuwa wakipewa pesa na DPW.
3) Hata kwenye mjadala wa leo, wabunge hao walikuwa wanapiga kelele badala ya kujibu hoja za Mpina. Wote kelele zao zimebakia kwenye kusema Mpina amedharau Bunge, amemdharau Speaker na Serikali, lakini hawakuijibu hata hoja moja ya Mpina.
4) Hili ndiyo bunge ambalo halijawahi kuchukua hatua zozote dhidi ya ufisadi unaoripotiwa na CAG kila mwaka.
Kwani ni nini cha kushangaza? Hivi kweli unatarajia mwovu aupige vita uovu? Tumeona mshikamano wa waovu. Laiti watu wema nasi tungekuwa na mshikamano kama walio nao waovu, nchi hii tungeweza kuikomboa kutoka kwenye mikono michafu.
KWA MPINA
Usisikitike wala kukata tamaa, bali ufarijike kwa kuwa umeunena ukweli utakaobakia kwenye kumbukumbu, na wananchi wote wenye uelewa na wanaolipenda Taifa lao wamekuelewa.
Haikutarajiwa watu waliofanya ufisadi kupitia sukari eti wangekuja hadharani na kusema kuwa kweli sisi ni mafisadi, kupitia huu uchafu wa mikataba ya sukari, tumetengeneza mapato yasiyo halali bilioni 36.
Kilichofanyika kwa sasa ni kuthibitisha tu kuwa uchafu uliofanyika kwenye mikataba ya kuleta sukari, haukuwa wa Bashe pekee, yumkini Bashe alikuwa mtekelezaji tu.
Huu ni uchafu sawa na ule wa EPA, Escrow na Kagoda, na ule ufisadi unaofanywa kila mwaka na kuthibitishwa na reports za CAG. Waovu wapo kwaajili ya kulinda uovu. Ni jukumu la watu wema kulikomboa Taifa lao.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA LAANA IKAWE JUU YA WEVI WOTE WANAOJINEEMESHA KWA MAPATO BATILI.
PIA SOMA
- News Alert: - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15
- Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili
- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge
- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia