Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 130
- 141
Kwa mara nyingine tena mwanamama Zainab Ansell Mkurugenzi wa Kampuni ya uwakala wa utalii nchini Tanzania ya ZARA TANZANIA ADVENTURE ,amenyakua Tuzo ya kampuni Bora ya Uwakala wa utalii Afrika ijulikanayo kwa Jina la 'Africa's Leading Tour Oparetor .
Tuzo hiyo imetolewa na World Travel Award's usiku wa kuamkia Oktoba 15 mwaka huu katika Falme za kiarabu ambako mama Zara aliambatana na mwanaye Leila ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo.
Tuzo hiyo sasa inaifanya Kampuni hiyo ya Zara Tanzania Adventure ya mjini Moshi kuwa Kampuni Bora ya Utalii Afrika kwa mara ya pili mfululizo ikifanya hivyo mwaka jana na mwaka huu ambako sherehe za utoaji wa Tuzo hizo zilifanyika Dubai .
Akizungumza baada ya Tuzo hiyo,Mama zara amewashuruku wadau wote waliochangia mafanikio hayo ikiwemo Wizara ya maliasili na Utalii,Bodi ya Utalii pamoja na mamlaka ya Hifadhi za taifa Tanzania(Tanapa) na sasa anaelekeza kampeni yake ya Twende Zetu Kilimanjaro katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambako kundi kubwa la wageni wanatarajia kupanda mlima Kilimanjaro kuanzia desemba tano hadi desemba 9 mwaka huu.