Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,885
- 9,272
Rais wa Senegal, Bassirou Faye amesema faida itakayotokana na mauzo ya mafuta na gesi "itasimamiwa vyema" wakati taifa hilo la Afrika Magharibi likianza kuzalisha mafuta kwa mara ya kwanza.
Kampuni kubwa ya nishati ya Australia ya Woodside imeelezea uzalishaji huo kama "siku ya kihistoria" na "hatuamuhimu" kwa kampuni hiyo na taifa la Senegal.
Mradi huo ulio kwenye kina cha maji cha Sangomar katika Bahari ya Atlantic ambako pia kuna gesi asilia, unalenga kuzalisha mapipa 100,000 ya mafuta kwa siku.
Ni mradi unaotarajia kuzalisha mabilioni ya dola kwa Senegal na kuchangia kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi wake.
Thierno Ly, meneja mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Petrosen, amesema taifa limeingia katika "zama mpya" kutokana na uzalishaji huo ulioanza rasmi jana Jumanne (Juni 11,2024).
"Hatujawahi kuwa katika nafasi nzuri hivi ya kupata fursa za ukuaji, ubunifu na mafanikio katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya taifa letu," amesema.
Petrosen ina hisa ya asilimia 18 tu katika mradi huo wakati Woodside inamiliki asilimia zilizobaki.
Rais Faye ambaye alichaguliwa kuongeza nchi hiyo mwezi Aprili, amekuwa na nia ya kujadili upya mkataba huo kamasehemu ya mageuzi aliyoahidi wakati wa kampeni zauchaguzi.