Hongera kwa mtu wa tatu, nchi sasa inaenda kupata mwelekeo

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
12,505
51,037
Kikwete, Magufuli na mtu huyu wa tatu...

Sasa ushahidi wote unaonesha mkulu kashindwa kabisa kuendesha nchi kwa ufasaha..

Ameshindwa Ku control hisia zake na kutofautisha cheo chake cha Urais na kuendesha familia au kuwa supervisor wa wizara.

Njia zote zilitumika kuamua kumuita kufanya naye suluhu hasa kwenye swala la Ukuta uliokuwa umeitishwa na Chadema.

Na aliwakatalia kata kata mashirika ya dini wakiwemo mashehe,Maaskofu,na wachungaji..

Sasa kwenye hili baa la njaa mtu huyu wa tatu baada ya kujua kabisa hali ya chakula ni tete na ni kweli kuna njaa kaamua kufanya Kazi yeye na kumuacha mkulu aendelee kuongea tu story zake za kijiweni kama alivyozoea baada ya kuona ashauriki.

Matamko ya Jana kutoka kwenye taasisi mbili kubwa za dini ni kielezo tosha kuwa mtu wa tatu kwa sasa ndiye anaendesha nchi kwa usiri mkubwa.

Matamko ya wakuu wa wilaya kukiri hatharani kuwa maeneo yao yana njaa ni ushahidi mwingine kuwa mtu wa tatu kaamua kufanya Kazi yake kwa usiri mkubwa ..

Mtu wa tatu kwa sasa ndiye anaedesha nchi maana mkulu akitaka kumfukuza mtu,lazima apitie kwake kuomba ushauri na hapo ndipo ufungwa speed gavana na huyo huyo mtu wa tatu...

Naziona dalili za mkulu kurudi kwenye mstari kutokana na ushauri wa huyu mtu wa tatu..

Mikutano ya siasa yote ya nje na ndani kurudi kwa kasi na kila kitu kuanza kuwa kama zamani....

Hivyo leo natoa pongezi kwa mtu huyu wa tatu kwa kufanya Kazi kwa weredi mkubwa .
 
Me sidhani kama kanisa Catholic ndo linaongoza nchi kwa sasa NEVER UNDER THE SUN..! balii wana Sheria kuna kitu kinaitwa "JUDICICIAL NOTICE" pale jambo linapokuwa wazi na halina haja ya kubishana huwa hairuhsiwi mtu ku argue.! Soo ni sisi wananchi ndo tunaoumia na Mhe. Ameliona hilo! We expect changes kwa Gvt juu ya baa hili la ukame
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…