Hoja za Tundu Lissu zazua mjadala Bungeni. Ni hoja ya mfumuko wa bei na njaa

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,873
11,123
Mimi ni mwana CCM, Linapokuja suala la uwezo wa Mtu na Akili kubwa huwa haki yake nampa mtu yeyote

Kama ninavyowashangaa wanahisabati na wana sayansi kama Albert Einstein, Isaac Newton na Blaise Pascal waliwaza nini na kwanini Walifikiria hivyo ndivyo kwenye siasa za Tanzania na amsha amsha huwezi kumuacha Tundu Lissu labda uwe una matatizo ya afya ya akili na stress za maisha.

Hoja za Tundu Lissu ziliwafanya watawala Wafute Bunge live, Tundu lissu Waziri akidanganya anasimama na kukuumbua peupe hivyo kufumbua macho wananchi kujua uwongo wa watawala.

Hoja za Tundu lissu ziliwafanya watawala Wafute mikutano ya siasa kukimbia aibu, Hoja ya kila mtanzania atapata Noah kwa gharama za fidia za madini, Lissu alisema report za kabudi ni rubbish na kweli miaka minne baadae kabudi amekiri walikuwa wanafanya uwongo kama mbinu ya kumridhisha mtawala

Kwanini nimeleta hoja hii hapa JF, Niliandika hapa mwaka jana https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1971739/

Mosi, Mfumuko wa bei haujaanza mwaka huu na wabunge wa ccm wapo lakini waliufyata mwaka wote uliopita wakisingizia vita ya urusi na ukraine

Tundu Lissu aliposema bei ya maharage na nyama hakuna utofauti kwa pasenti ya kuongezeka kuna mamluki nje ya Bunge wakaja na bei zao eti hakuna bei ya mchele ya Tzs 3,500 bali kuna Tzs 1,800 na aliyesema haya alishatenguliwa Kitengo cha Propaganda amepelekwa Morogoro vijijini akasuluhishe vita ya wakulima na wafugaji.

Mwana ccm mpya Bashiru Ally Leo analalamika bei ya vitu kupanda, Mwaka jana watu walipolalamika tozo inaumiza maisha ya wananchi waliufyata kimya huku mmoja akitaka Wanaolalamika maisha màgumu wahamie nchi jirani ya Burundi.

Ni muda muafaka kama Taifa watu wenye uwezo mkubwa kuwa kubali na kuwapa heshima yao kwa mawazo yao na michango yao.

Haya mambo ya kuwa chawa ndio matokeo ya wabunge vigeugeu.

Tulisema vita ya Ukraine na Urusi haitaisha Leo wala kesho hivyo kwa mipango ya muda mfupi kisingizio kutakuwa Vita lakini kwenye mipango ya muda mrefu kisingizio cha vita hakina mashiko tena.

Bila Kuongeza uzalishaji na kutoa ahueni kwa wakulima, gharama za maisha zitaongezeka mwaka hadi mwaka.

Mchawi wa mfumuko wetu wa bei ni kushuka kwa uzalishaji, Tusitafute mchawi ni nani.
 
Mchawi wetu ni CCM na serikali yake kwani wao kazi kubwa wanayoifanya kwa bidii ni ya ufisadi tu. Nambie kama unajua kiongozi yeyote wa CCM asiyekuwa mwizi
 
Mchawi wetu ni CCM na serikali yake kwani wao kazi kubwa wanayoifanya kwa bidii ni ya ufisadi tu. Nambie kama unajua kiongozi yeyote wa CCM asiyekuwa mwizi
Tatizo baadhi ya wabunge wanasifia tu
 
Back
Top Bottom