Hizi ni Nchi zinazotoa VISA bure, Wabongo tunafeli wapi kusongamana ughaibuni kama Wanaijeria

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,818
5,420
Wabongo nyoso ni wananchi ambao hawana desturi ya kusafiri nje ya nchi. Wote tumesongamana hapa Nchini utafikiri watoto wanaosubiria nyumba ya urithi.

Nchi zinazotoa VISA ya bure kwa Watanzania.

View: https://www.instagram.com/p/CxC5PRyuwra/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

Japokuwa Nchi yetu inashika orodha ya idadi kubwa ya Raia ambao ni zaidi ya milion 60, na kwa Afrika mashariki ndio vinara wa idadi kubwa ya raia, ila hatuna watu wengi wanaotoka nje ya nchi.

Moja wapo ya sababu nchi yetu sio maarufu Duniani kote kama Wanaijeria, wasauzi na Wakenya, ni kuwà Nchi yetu Raia wake sio wengi ughaibuni.

Ukienda nchi za wenzetu Wabongo unaweza kuwatafuta kwa Tochi na usiwapate. Hizo hapo juu ni nchi ambazo huitaji kibali cha Visa kuingia kwao, Yani ni wewe na nauli yako na passport yako basi.

Sasa unakuta na Nchi ni ya Free VISA ila Wabongo bado huwakuti. Hii ni shida sana, na hizi fursa za free VISA watu kama Wanaijeria uwa hawazichezei kabisa.

Ndio maana naijeria ni nchi maarufu duniani kwa sababu Raia wake wametapakaa na kuitangaza nchi hivyo hivyo kwa wasauzi na Wakenya.
 
LUGHA
LUGHA
LUGHA
LUGHA
LUGHA
Yeah lugha inaweza kuwà na impact lakini si hipi uzito kwa sababu... Mimi nimewahi kukutana na Mnaijeria jijini Mwanza, yupo kwenye Vibanda vya kubetia anabeti na hajuhi kiswahili, na anaowaongelesha nao ni wa kiingereza cha kuungaunga. Mbona Wachina, Wahindi, Wabelgiji, waarabu na watu wamataifa mengi yasiyo ya kiingereza wanakuja bongo na wengine hawajui hata kiingereza, wanakaa wanaanza kujifunza mdogo mdogo kiswahili kwa kuunga unga. Kwa nini tusiwe wa kama wao... Mbona sauzi tunasongamana na wasauzi hawajui kiswahili na tunaishi nao... Kwa nini Tusiende mataifa mengine tukafanya hivyo hivyo
 
Wabongo nyoso ni wananchi ambao hawana desturi ya kusafiri nje ya nchi. Wote tumesongamana hapa Nchini utafikiri watoto wanaosubiria nyumba ya urithi.

Nchi zinazotoa VISA ya bure kwa Watanzania.

View: https://www.instagram.com/p/CxC5PRyuwra/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

Japokuwa Nchi yetu inashika orodha ya idadi kubwa ya Raia ambao ni zaidi ya milion 60, na kwa Afrika mashariki ndio vinara wa idadi kubwa ya raia, ila hatuna watu wengi wanaotoka nje ya nchi.

Moja wapo ya sababu nchi yetu sio maarufu Duniani kote kama Wanaijeria, wasauzi na Wakenya, ni kuwà Nchi yetu Raia wake sio wengi ughaibuni.

Ukienda nchi za wenzetu Wabongo unaweza kuwatafuta kwa Tochi na usiwapate. Hizo hapo juu ni nchi ambazo huitaji kibali cha Visa kuingia kwao, Yani ni wewe na nauli yako na passport yako basi.

Sasa unakuta na Nchi ni ya Free VISA ila Wabongo bado huwakuti. Hii ni shida sana, na hizi fursa za free VISA watu kama Wanaijeria uwa hawazichezei kabisa.

Ndio maana naijeria ni nchi maarufu duniani kwa sababu Raia wake wametapakaa na kuitangaza nchi hivyo hivyo kwa wasauzi na Wakenya.

Zaidi ya HongKong na Singapore, hakuna nchi za maana.
 
Mazoea na nauli mtihani.south unaweza zamia hata kwa miguu na Sio kwa weupe bila milioni Tano ujafika ulaya.
Sasa milioni Tano bongo ni mtaji tosha.
Labda bodi ya mikopo iache kuwakopesha elimu iwakopeshe nauli vijana watarejesha wakianza kubeba box.
 
Back
Top Bottom