1. Awareness – of why the change is needed
Kufahamu sababu ya kuhitajika kwa mabadiliko nchini (Lazima sababu iwepo) kama hakuna sababu basi hayo si mabadiliko bali ni komedi.
Kwa bahati mbaya kumekuwa na hisia hasi kuwa maendeleo ni kijamii na kiuchumi pekee, pasipokufahamu hata maendeleo kisasa ni mhimu pia kwakuwa Rais, wabunge na madiwani nk. hupatikana kwa njia ya kisiasa.
2. Desire – to support and participate in the change
Hii ni hatua ya pili ambayo ni uungwaji mkono na ushiriki wa wananchi katika mabadiliko yaliokusudiwa. Kama hakuna uungwaji mkono wa wananchi walio wengi basi hayo si mabaliko, bali ni sanaa kama zilivyo sanaa zingine duniani.
3. Knowledge – of how to change
Maarifa ya namna ya kufanya mabadiliko. Hii ni hatua ya tatu ambayo huitaji maarifa zaidi kuliko hisia za mtu/watu wachache tu. Hii huzingatia zaidi hali halisi na uzoefu wa watu kwa mda mrefu kabla ya kufanya uamzi stahiki. Kama hakuna maarifa zaidi basi mabadiliko yataendelea kusikika katika vyombo vya habari vya nchi za ughaibuni.
4. Ability – to implement new skills and behaviours
Uwezo wa kutekeleza mbinu na tabia mpya. Hii ni hatua ya nne.
Hii huzingatia uwezo wa watu husika katika kutekeleza mambo mapya. Iwapo hakuna watu hao bali ni watu walewale basi kuwa na mabadiliko ni ndoto kama zilivyo ndoto zingine tu.
5. Reinforcement – to sustain the change
Msukumo wa kuendeleza mabadiliko yaliyopatikana. Hii ni hatua ya tano na mhimu sana. Hii hasa inahusu kuwekwa kwa hayo mambo yote katika katiba au kuyatengenezea kanuni, taratibu au sheria kama mwongozo. Kama kumefanyika mabadiliko na hayo mabadiliko hayapo katika katiba basi hayo si mabadiliko bali ni hadaa kama zilivyo hadaa zingine duniani.
NB: Unafikiri kama Taifa tumekwama katika hatua ya ngapi?
Karibu kwa mjadala huru.