Hizi ndio Tabia za Mzalendo

Joseph Nyoni

Member
Apr 21, 2024
5
2
TABIA ZA MTU MZALENDO

Na Joseph Nyoni

Uzalendo nini? Uzalendo ni ibada ya kulipenda, kulitumikia na kulitetea taifa katika hali yoyote pamoja na kutanguliza maslahi ya taifa.

Zifuatazo ni tabia za mtu mzalendo

1. Analipenda taifa lake na hawi tayari kuliona taifa lake linaingia kwenye shida, matatizo au linaonewa, linaaibika na kunyanyasika, muda wote anaangalia faida/ maslahi ya taifa lake.

2. Kulipigania taifa linapoingia katika dhiki, shida, na kila hali

3. Mzalendo si mbinafsi! Hatangulizi mambo yake bali ya taifa. Taifa lifaidike kwanza yeye baadaye. Tuliwaona akina Hayati J.K Nyerere, Karume, na Sokoine.

4. Popote akiwa ndani au nje ya taifa atasimama kulitangaza taifa lake akijisikia fahari hata katika aibu atakubali kuibeba kwaajili ya taifa lake.

5. Mzalendo si mbaguzi, havai vazi la udini wala ukabila, anavaa vazi la taifa. Hawezi kubagua ngozi wala jinsia.

6. Anajivunia taifa lake

7. Atafundisha watu kulitumikia taifa

8 Ataheshimu maoni chanya ya kila mmoja katika kujenga na kulitumikia taifa

9. Atapenda na kuheshimu haki za wengine katika taifa

10. Mzalendo lazima atalitumikia taifa kwa kufanya kazi fulani katika taifa lake.

11. Atafichua wezi, wala rushwa na mafisadi katika eneo lake analoishi au analoongoza.

12. Atakuwa jasiri (Ili uwe ngao ya kulitetea taifa sharti uwe jasiri)

13. Ataandaa/ atafundisha watoto na vijana kutetea taifa

14. Ataweka mbele utamaduni wa taifa lake

15. Atalitangaza taifa lake mbele ya mataifa mengine

16. Atatetea rasilimali za nchi

17. Atapinga unyonyaji na ukupe (Uchawa) kwani ni chembe ya unafiki na kula kwa kutegemea unyonyaji na unafiki.

18. Atahamasisha jamii yake kuelekea maendeleo makubwa

19. Atatoa mawazo ya kulijenga taifa.

20. Hatokubali kuwa tegemezi wa mtu au kitu bali kujitengenezea nafasi ya kujitegemea mwenyewe.

21. Atafikiria kizazi kijacho cha taifa kuliko anavyofikiria vizazi vya familia yake.

Na Joseph Nyoni
0766875334
 
Uzalendo ni pamoja na kupenda na kupigania Usawa na sio kufurahia Wizi wa Kura unaofanywa na CCM.
 
Mzalendo syo mtu wa kujilimbikizia mali
Life style yake tu anayoishi utajuwa huyu mzalendo

Ova
 
Kunatofauti kati ya Chawa na Mzalendo katika Tanzania ya sasa,

Kwanza, Sifa ya chawa ni kusifia mtu au watu kwa vitu wanavyomiliki kwa mfano magari,nyumba,Pesa,Uzuri,Kupendeza etc

Pili, Sifa ya Mzalendo ni kusifia record za mtu au watu na mfano wa hizo record ni kama , Ushujaa wa mtu kwenye kupinga rushwa, Uonevu, Ufisadi, Uzembe na Matendo mengine mabovu.

Tatu, Chawa anatafuta faida yake wakati Mzalendo anatafuta faida ya Taifa au nchi kwa ujumla wake.

Je, wewe ni chawa au mzalendo?​
 
Kunatofauti kati ya Chawa na Mzalendo katika Tanzania ya sasa,

Kwanza, Sifa ya chawa ni kusifia mtu au watu kwa vitu wanavyomiliki kwa mfano magari,nyumba,Pesa,Uzuri,Kupendeza etc

Pili, Wakati Mzalendo anasifia record za Mtu au watu na mfano wa hizo record ni kama , Ushujaa wa mtu kwenye kupinga rushwa,Uonevu,Ufisadi, Uzembe na Matendo mengine mabovu.

Tatu, Chawa anatafuta faida yake wakati Mzalendo anatafuta faida ya Taifa au nchi kwa ujumla wake.
Umejitahidi sana kufafanua ila umesahau chawa ni mtu wa hovyo hovyo tu anaesifia vya uongo ilimradi apate chochote kitu.
 
Kuwa Mzalendo na uchungu na nchi yako maana yake, uwe chawa wa Viongozi, kila kitu uwe unasifia tu, kuwatetea Viongozi wako hata kama wamenakosea?
 
Back
Top Bottom