Hizi ndio sababu zinazofanya wanawake wasitamani kuolewa

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
19,168
37,182
Habari za wakati huu huu wandugu na majamaa.....

Siku hizi imekuwa ni jambo la kawaida kukuta mwanamke yupo singo hata katika umri ambao angetazamiwa kuwa ameshaolewa....

Au imekuwa ni kawaida kukuta mwanamke akiwa na mtoto au watoto huku akiwa peke yake....na wengi wao huonekana wanafurahia hali hiyo.....hili jambo wadau wengi wa masuala ya kijamii wamekuwa wakilielezea kuegemea upande wa kuwalaumu wanawake tu kana kwamba ni watu wenye tabia mbaya na hizo mimba walijipa wenyewe.....

Kiukweli hii hali haikujitokeza tu kwa bahati mbaya au kwa kuzuka tu....hii ni hali ambayo kwa namna fulani imeundwa na hali ya wanaume kuyakataa au kuyakimbia majukumu yao.......

Iko wazi kuwa miaka hii au zama hizi wanaume wamepoteza sifa na sababu za wao kuwa viongozi wa familia kwa kuwa na upeo mdogo wa kukabiliana na majukumu ya kifamilia......hata humu kuna kesi kibao za vijana wa kiume wakiomba ushauri kuhusu familia zao katika masuala ambayo mtu hata kwa akili ya kawaida mtu unashindwa kuelewa kuwa kama baba wa familia anashindwa kutatua suala dogo kama hilo je hiyo familia anaiendeshaje....???

Miaka ya nyuma ilikuwa ni jambo la kujivunia kwa mwanamke kuolewa na kuwa na familia yake na lilikuwa ni jambo la kishujaa kwa mwanamume kuweza kumudu kuihudumia familia yake katika mahitaji yao yote ya msingi...

Kwa familia ilikuwa ni fedheha kwa mtoto wao wa kike kutokuolewa...lilikuwa ni tukio la kuwafanya wazazi au wanafamilia waende mbali zaidi hata kwenye mambo ya kishirikina yote ni kutafuta kujua kwanini binti yao haolewi.......

Lakini nyakati hizi kutokana na mienendo mibovu ya wanaume kwenye ndoa imewafanya wanawake wasione umuhimu wa kuwa na mume achilia mbali kuishi na mwanamume......

Kila kukicha vyombo vya habari vinatawaliwa na habari za mwanamume kumfanyia mkewe ukatili usioelezeka......

Kila siku wanawake wanasikia habari mbaya za wakina mama wanaoteseka kwa mateso baada ya kutelekezwa na waume zao.....

Kila uchao kunazuka taarifa za vijana wanaokataa mimba au wanawake wanao pata maradhi baada kuchukua maamuzi ya kutoa mimba baada kusalitiwa na wale waliodhani ni wenzi wao(wanaume)

Katika mazingira kama hayo unategemea kuna mwanamke gani mwenye ujasiri wa kuwa na hamu ya kuingia kwenye ndoa...ikizingatia kuwa wengi wao wanajiweza kiuchumi.......

Hali iliyopo ya wanawake kutaka kuwa sawa na wanaume ni kutokana wanaume kuyakimbia majukumu yao na kuwaachia wanawake.....na huu ni udhaifu mkubwa sana ambao wanaume tunauonyesha....kwa wanawake....

Fikiria kuwa ikiwa mwanamke anamudu gharama za kuitunza familia na kuipatia mahitaji yote ya msingi baada ya kutelekezwa na mumewe ataachaje kujiona sawa na mwanaume ikiwa majukumu yote ya mwanaume kwenye familia anayafanya yeye mwenyewe na kuyamudu....???

Nisiendelee mbali ila ninachowakumbusha wanaume wenzangu turudi kwenye mstari na tusimame kwenye majukumu yetu na kuyatiniza ipasavyo kamwe hutasikia wanawake wakidai usawa....kwa huo usawa utafunikwa na huduma atakazopewa na mumewe.......

Nawasilisha......
 
umenena vyema kabisa unakuta mwanaume analalamika kabisa kuhudumia familia yake .. kweli mtani leo unena vyema
 
Utegemezi wa mwanamke na mwanaume una utofauti mkubwa sana... Mwanamke anategemewa na familia yake tu, ila mwnaume anatagemewa na ukoo/jamii nzima... ni majukumu magumu na mazito sana...
 
Hahahaaa! Kikulacho chako, hapa umeenda malkiti mkuu, unggelezea pande zote mbili. Nikianza na wanawake. Haya ya kutoolewa wao ndio chanzo kujifanya wajuaji,jeuri na usasa ndio unawafanya waishie kuzalia nyumban, wanawake sasa hivi kutembea na wanaume watano kwa wakat mmoja ni fassion yao, mtu ana mchumba wake lakin huku anagalagazwa na wengne kama 6 nani wakat huo anajazwa mimba na hao wa nje na anakusingizia kuwa mimba ni yako hapo kosa la nani?

Dharau kibri kutaka kujifanya nayeye mbabe hayo ndio yanayowaponza.

Nikija kwa wanaume: wanaume ni kweli wanakwepa majumuku wengi hawajielewi ule uwezo wa kuuumiza kichwa namna ya kuongoza familia haupo tena,.

Hitimisho: Wanawake badiliken jiheshimuni hayo ya kujifanya uchi wenu ndio mitaji inawaponza, kujifanya uzuri na mvuto upo kwenye uchi inawaponza. Mtazeeshwa mkiwa nyumban
 
Umenena vyema mkuu, sikuhizi sio jambo la kushangaza kuona single mothers kibao mtaani, but zamani ilikua ni ishu.

maisha yamebadilka, wanaume hawataki tena majukumu yao hasa akiona mkewe ana kazi ndo kabisaaaa, yan hajishughulishi au anatoa akijisikia so lazima mama akudharau kwakua umejishushia heshima mwenyewe.

kwa wasio oa pia hali si nzuri sana, vijana wanapenda maisha mazuri mjini but kujituma zero no wonder idadi ya mashoga inaongezeka kila leo kwa kupenda vya bure
 
Hawa watu wanaotetewa baadhi yao wamekuwa pasua kichwa ile mbaya....Ukijichanganya tu huna bahati
 
mmmmh msiwe mnaongea tuu ili kuwa favor watu fulani!
Kwanza dadaz wengi wanajifanya wajuaji mtaani kutwa wanalia hawaolewi,hapa only the the best will be selected ukiwa jeuri utaishia kuolewa unafukuzwq asubuh,
Na pia wanaume wanazaliwa wachache 2/10 na hii lifestyle ya one woman one man mliorith kwa wazungu ndio inawa cost ingekuwa enzi hizo ni 35/1 wooote wangeolewa
Unakuta mtu ana mke na vimchepuko viwili kila cku analipia guest 7500 sasa c bora aoe tuu awe nao watatu
 
Uzinzi tu ndio wanaendekeza, Mungu hakutaka iwe hivi ilivyo sasa, shetani tu ndio anawapeleka watende na kuvunja amri ya Saba
 
Mkuu umeegemea upande wa wadada peke yao,kwa taarifa za uhakika hilo lipo pande zote,sasa hv kuna wanawake humu mjini ni bola ukutane na nyoka mwenye sumu kali kuliko hao wanawake,sema mtu huongea kitu ambacho hakiawah mtokea au kuona nduguye akipatwa na masaibu ya hawa wanawake wa mjini washindao salon na kwenye tamthilia,kwa ufupi kuna wanawake washenzi na zaidi ya washenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…