Hizi kelele zinazopigwa na baadhi ya watu dhidi ya ujenzi wa Tanzania Mpya hazizuii lengo

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Tunaendelea kujifunza kwa watu waliofanikiwa na viongozi wetu waliotutangulia kuanzia kwenye vitabu vitakatifu hadi waasisi wa Taifa Letu kuwa ujenzi wa Taifa Imara sio lelemama na wala sio Kula na Kunywa bali ni kufunga mkanda na kujikana wenyewe kwa kuchagua Dira sahihi tunayotaka kuifuata. Katika hili Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ina dhamira ya dhati ya kuijenga Tanzania yenye neema. Hili halina Ubishi, Rais wetu ameamua na anasonga mbele hakuna wa kuzuia Safari ya Tanzania Mpya kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa katika Hotuba zake kuwa Kupanga ni kuchagua, Mafanikio hayaji kwa kupiga domo ila kwa Kufanya Kazi, ni muda wa kazi kwa kwenda mbele. Kila mtu anajua hata kama vyura wanapiga kelele nyingi kiasi gani Tembo lazima anywe maji hakuna namna, Tanzania Kwanza.

 
Safi Sana mkuu Maada yako nimeipenda

Mfano mzuri Hawa wabunge ETI hadi wa upinzani wakajifanya wanatetea wauza unga mara ooh wameonewa
Uzuri ni kwamba kelele zao hazina nguvu za kuwayumbisha makonda na magufuli. Kwanza Sana tanzania inapiga hatua Sana kwenye hii vita tunamshukuru MUNGU tumewajua wapiga kelele wetu
 
Mkuu..kupanga ni kuchagua....na sio kila linapangwa na kuchaguliwa ni jema kwa mstakabali huo.
....inategemeana sana genge la waliokaa kupanga hiyo dira kama wana uono murua(illuminated).... kama uvuvio wao ni hafifu ni lazima tutadumbukia shimoni.

.....ni hayo tu kwa leo-twende zetu kule group letu la diaspora nnkamu gwangu.
 
[QUOwa jabulani, post: 19758821, member: 313923"]Utakuwa wa chato wewe.[/QUOTE]
Sio wa Chato hata kidogo...ameeleza hisia na mtazamo wake...tumpinge kwa hoja.
 
Vumilia bado kidogo utaelewa usiwe na haraka!

Mwizi lazima amtetee mwizi mwenzie.Hakuna cha kwenda mbele hapo ni tumerudi nyuma hatua alfu.

Nyumba yetu sote kwanini tusijenge wote??Kwani mnatuficha nini??Kwanini hamtaki kukosolewa.

Any way pole naona mkirudi 2020 tutawaambia hatuna mashamba ya kura
 
Tanzania mpya tumeanza kuijenga lini? na itajengwa kwa miaka mingapi? Nchi yetu iko huru kwa zaidi ya miaka 50, then leo ndio tunataka kuanza kujenga Tanzania mpya? hiyo miaka mingine 50 tulikuwaga tunafanya nini? Nyie majamaa acheni propaganda zenu za kitoto.
 
Kuna watu hawawezi kukubali kwa sababu Tanzania ikitaka kujikwamua kutoka hapa ilipo kwenda mbele kuna watu wanaumizwa..mfano mdogo ni kwa bwana mbowe mwenyekiti wa chadema..ye amekuwa mmoja wa wahanga wakubwa katika mabadiliko maana alizoea kufanya zake biashara bila kulipa kodi hakuna aliyemghasi..alizoea kulima kwenye vyanzo vya Maji hakuna aliyemghasi..leo hii amedakwa kila sehemu..sasa unadhani mtu kama huyu na familia yake na wafuasi wake watafurahia mabadiliko halisi ya nchi ukitoa yale ya hands rotating..
 

hivi kile kiwanda cha ku-manufacture magari tulichoambiwa kingeanza production december 2016 kimeishia wapi?
 
 
Aliyeshindwa kujenga nchi kwa miaka 50 toka 1961 anajaribu kuanza kuijenga 2017 halafu anataka watu waamini kuna matokeo chanya yanakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…