Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,995
5,227
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inawatangazia taarifa ya maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora.

Nauli hizi ni baada ya kufanyia kazi maombi yaliyoletwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) na taarifa zilizopokelewa kutoka TRC na wadau wengine.

Kuelekea kuanza kwa safari za SGR Dar es Salaam mpaka Makutupora, masharti ya kuzingatia kabla ya kuanza kutumika kwa nauli hizi ni kama ifuatavyo:

(i) Mtoa huduma (TRC) kuwa na leseni ya usafirishaji:
(ii) Kuwa na ithibati ya usalama wa miundombinu ya reli na mabehewa;
(iii) Kutumia mfumo wa utoaji wa tiketi za kielekroniki;
(iv) Kuunganisha mfumo wa tiketi za kieletroniki na mifumo ya LATRA;
(v) Kukokotoa malipo na utunzaji taarifa za abiria, nauli iliyolipwa, tiketi za kielektroniki zilizotolewa, kodi za Serikali na tozo za kisheria; na,
(vi) Kuwa na watumishi wa kada muhimu kwa masuala ya ufundi na uendeshaji wa treni ya SGR ikiwa ni pamoja na madereva waliothibitishwa na wahudumu waliosajiliwa na LATRA.

Aidha, nauli hizi ni kwa daraja la kawaida kwa watu wazima na watoto kuanzia umri wa miaka 4 hadi 12 ambapo nauli zitalipwa na abiria kwa kilomita. Nauli itakayolipwa na mtu mzima na mtoto mwenye umri zaidi ya miaka 12 ni TSH. 69.51 kwa kilomita, na mtoto kuanzia kuanzia miaka 4 hadi 12 atalipia TSH 34.76 kwa kilomita. Aidha mtoto mwenye umri chini ya miaka minne (4) hatalipa nauli, hata hivyo, taarifa zao na wasafiri wote zitatunzwa kwenye mfumo wa taarifa za abiria wanaosafiri kila siku.

1718044353764.png

1718044376285.png

1718044390131.png
 
View attachment 3014035
View attachment 3014036
View attachment 3014037
Ksbls ys yote semina elekezi itolewe watu wataanza kuchafua kukojoa na haja kubwa hovyohovyo mabehewa yakaanza kunuka
 
Nauli nzuri mno, mimi napenda watuambie safari ngapi kwa siku! Tunataka asubuhi tuwe tunaenda Dom , mchana tunakula bata kisha usiku saa 6 tupande treni ya express kurudi Dar. Treni za kusimama kila kijiji hatupendi, wengine tumezaliwa town huwa tunaboreka sana kutuweka bush masaa kadhaa.
 
Back
Top Bottom