KERO Hizi gari za Kakola kwenda Kahama na Kakola kwenda Geita hazifai

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
713
1,189
Siyo kwamba Traffic haziona la hasha wanaziona na wanaingia Hadi ndani mwezi wa kwanza mwishoni nimepanda gari ya kwenda Geita ikitoka kakola hiki ndo nilicho jionea!

Kwanza unapotola tu stend ya kakola unaukaribia shule ya secondary Buly.

Hapo Kuna Traffic pamoja na askari wapo pale daily.

Cha ajabu watasimamisha gari na kukuwaambia abria fungeni mikanda Ili Hali wengine wamesimama.(kituko)

Ndani ya basi siti zimechoka huwezi amini na zingine zimeng'oka kabisa na ni hazard muda wowote zinaweza leta madhara zikichangia na njia sio salama!

Unapoingia lami tu barabara ya nyakumbu ulitokea kakola pale Kuna matraffic si chini ya 6 daily na wao wimbo ni ule ule fungeni mikanda huku wakiona live Kuna baadhi ya abria wamesimama.

Pia hapohapo nyakumbuku Kuna muda utakuta abiria walio simama wanashushwa wanapakiwa kwenye bajaji hata3-4 then wanaenda Hadi mbele Kuna shule ya jina limenitoka.

Gari ikifika hapo itasimama na kusondoka watu kama mkaa sio kwamba traffic hawajui la hasha wanajua sana.

Hii tabia ya kufaukisha abiria imedumu sana Kwa miaka kadhaa Hadi Sasa na ni eneo hilohilo.

Niwaulize ninyi Traffic wa geita na kakola mnapewa Nini na Hawa wamiliki wa magari ya abiria ? Mbona mnaweka maisha ya watu hatarini ?

Kazi yenu hasa ni Nini ?

Hizi ni baadhi ya siti ya gari Moja wapo ya kakola to Geita. Gari hizi sio salama Kwa kusafirisha abiria.

Tunawaomba idara husika mliangazie hili.

IMG_20240125_185641_640.jpg
 
Barabara ina mashimo na mbavu za mbwa mwanzo mwisho hakuna tajiri atapeleka gari luxury

Tatizo sio trafiki wala tatizo sio wenye magari tatizo ni barabara

Hiyo barabara ya kahama Geita ingekuwa na Lami gari za abiria zingekuwa za kutosha barabarani na hakuna mtu angesimama!

Geita imeshatelekezwa kwa upande wa miundo mbinu
Naweza kusema Geita ndiyo mkoa pekee ulioko kwenye top 10 ya mikoa inayoongoza kwa mapato lakini miundo mbinu yake ni mibovu haswa!.
 
Mleta mada ungejitahidi kutueleza ubora wa barabara, yawezekana ni sehemu ya tatizo, wamiliki wa vyombo vya usafiri wa abiria hupendelea kupeleka magari kwenye barabara nzuri, yakichoka huko ndio yanasogezwa kwenye barabara za huko
 
Huko kuna shida tena kubwa mwaka jana kuna gari huwa inakipindia sppend isiyo ya kawaida coster hiyo inaitwa mkono inaongoza kwa kupata ajri na kugonga watu na kuua .

kuhusu malalamishi ya mtoa mada nikweli gari zimechoka sana hasa siti lkn barabara pia ni mbaya sana njia nzuri ni geita to msalala karumwa. Barabara hiyo ndo nzuri japo ni ya vumbi.

Binafsi niliwahi panda nikitokea bugarama kwenda geita ilikuwa majira ya 12 jioni hadi tunafika nyakumbu geita saa5 kasoro.

tumeenda hadi nyarugusu tumeenda kabisa mbele kuna kijij kama kuna njia panda vile tunaambiwa njia haipitiki kule hivo inatubidi turudi tena sijui kuna sehemu inaitwa nyakagwe karibu na geita asee njia ilikuwa mbovu sana na gari nalo bovu siti zimeng'oka halitamaniki aswee kuna sehemu watu wanateseka sana.

cha kushangaza kakola inamgodi mkubwa tu wa dhdhabu pale bukoli kwa mbele kuna mgodi mdogo nao tulikuta watu kibao pale wakifanya shughuli za uchimbaji ukienda hapo nyarugusu ni machimbo ya miaka na miaka lkn barabara ni mbovu ajabu geita ni bonge la mgodi. serkali jaribuni kuangalia eneo hilo. Uchuymi upo vizuri sana anga hizo lkn cha ajabu lami ipo geita pekee kakola pale kuna kipande cha lami hakifiki km3 inachekesha sana
 
Mleta mada ungejitahidi kutueleza ubora wa barabara, yawezekana ni sehemu ya tatizo, wamiliki wa vyombo vya usafiri wa abiria hupendelea kupeleka magari kwenye barabara nzuri, yakichoka huko ndio yanasogezwa kwenye barabara za huko
barabara ni mbovu sana ile japo kwasasa siko maeneo hayo.mleta uzi kapotea
 
Barabara ina mashimo na mbavu za mbwa mwanzo mwisho hakuna tajiri atapeleka gari luxury

Tatizo sio trafiki wala tatizo sio wenye magari tatizo ni barabara

Hiyo barabara ya kahama Geita ingekuwa na Lami gari za abiria zingekuwa za kutosha barabarani na hakuna mtu angesimama!

Geita imeshatelekezwa kwa upande wa miundo mbinu
Naweza kusema Geita ndiyo mkoa pekee ulioko kwenye top 10 ya mikoa inayoongoza kwa mapato lakini miundo mbinu yake ni mibovu haswa!.
naunga mkono hoja

hiyo geita kahama na kakola kiuchumi wapo vizuri sana chaajabu miundondo mbinu ya kakola na geita ni 0
 
Mleta mada fursa hiyo kanunue gari zako nzuri peleka kwenye hizo njia

Traffic unataka wafanyaje? Wapige marufuku hizo gari mbovu watu watapanda defender za polisi? Kwa ajili ya usafiri?
 
Back
Top Bottom