Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,626
- 13,847
Kwa mara ya mwanzo vikosi vya Hizbullah nchini Lebanon vimetoa tangazo la kuzirushia makombora ndege za kivita za Israel na kuzilazimisha kurudi zilikotoka.
Kufuatana na taarifa ya aljazeera makombora ya kusaka ndege kutoka ardhini kwenda hewani yametumika kuzilenga ndege hizo ikiwa ni siku moja tu baada ya kamanda mkubwa wa Hizbullah kufa kutokana na shambulia la Israel.
Katika historia ya vita baina ya Israel na Lebanon vikiongozwa na Hizbullah,kundi hilo limewahi kuvipiga vifaru kadhaa vya Israel na mwaka huu kuzidungua droni kadhaa za Israel.Hata hivyo bado hawajahi kuiangusha ndege ya kivita ya adui yao.
Kuzipiga ndege za kivita ambazo huruka kwa kasi kubwa na uwezo wake wa kuruka mbali angani ni jambo linalohitaji kumiliki silaha bora kwa ajili ya shughuli hiyo..Ukossefu wa silaha za aina hiyo kwa upande wa Gaza ndiko kulikopelekea watu wengi kufa na majumba kubomolewa bila kizuizi.
Kwa vyovyote vile vita vya muda mrefu baina ya Israel na majirani zake kutapelekea kila mmoja kutafuta silaha zinazoendana na uadui wanaofanyiwa na taifa hilo.