Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,567
- 158,296
Wanawake hawapendi kuchosha ubongo wao kwa kujisomea au kujiombea au kufanya mambo binafsi, ndio maana kila kanisa zuri yupo, kila nabii mzuri yupo, kila maombi anataka aombewe yeye.
Ukiwa kanisani mchungaji akiita watu watoke mbele unakuwepo Wagonjwa waje niwaombee na wewe umoooo. Wakati hunywi maji yakutosha. Hulali kwenye chandarua. Humezi dawa za minyoo.
Wenye madeni watoke mbele niwaombee na wewe umo. Mchungaji wako mwenyewe kiwanja cha kanisa alikopa na analipa mkopo kwa wakati. Hata kama wewe ni mdogo wake wa TB Joshua kanuni za pesa zinakutaka kulipa deni na sio kumuombea mwenye deni asahau au afe.
Wanaotaka kufungua biashara watoke mbeleee na wewe umo. Hujawahi hata kuuza genge unataka kufungua super market. Hujafanya hata research ya biashara unayoiwea lakini unataka kuwekewa mikono.
Wenye kutaka safari za nje ya nchi toka mbeleeee na wewe umoooooo. Passport yenyewe huna. Kijijini kwenu kwenyewe una miaka mitano hujaenda kusalimia wazazi lakini unataka kwenda Ulaya.
Wanaoteseka kwenye ndoa watoke mbeleee na wewe umoooo. Kisirani huongei na mumeo vizuri. Sio msafi, humpikii mumeo japo kwa wiki mara moja. Hujuagi hata kama boxer zake zimetoboka. Hujui hata mumeo leo kama amebeba kitambaa cha kujifutia lakini bado unataka kuombea
Wanaotafuta kazi watoke mbele niwaombee na wewe umoooo. Hujawahi hata kuandika maombi ya kazi. Huna hata mpango wa kujiajiri kwa elimu yako.... Huwezi hata kujitolea kufanya kazi bila malipo.... Hujawahi hata kutembea kwenye maofisi matano ukapaeleka barua zako kutwa uko kanisani unaombewa yaani upate kazi kwahiyo unataka kazi ikufuate hapo kanisani?
Wanaoota ndoto mbaya usiku watoke mbele niwaombeena wewe umoooooooo. Kutwa umeshinda na kisirani. Kutwa una hofu ya kushindwa. Kutwa nzima unawaza mambo mabaya sasa unataka usiku ukiingia uote nini? Uko mbinguni na malaika? Wakati siku nzima ulikuwa na maushetani tuu
Wanaotaka viwanja vya kujenga aaa na wewe umooooooo. Chumba ulichonacho tuu hukipendi huwezi hata kupaka rangi. Huwezi hata kupanda maua eneo lako. Huwezi hata kupafagia pakaeleweka, je hiyo nyumba utaifanyaje?
Wanaotaka magari watoke mbele niwaombeeeee na wewe umooooo. Hujachukua japo hatua ya kusomea udereva. Hujawahi hata siku moja kwenda pale showroom ukaulizia japo bei. Hujawahi hata kwenda garage ukidadisi mafundi na kujua changamoto za wenye magari...ila unataka gari sasa ata ukilipata si utaliuza tuu mwanamke?
Waliiomba mkopo ukagoma watoke mbele niwaombee na wewe umooooooo. Una madeni kila kona na yote unasumbua kuwalipa wenyewe bado unatoka kwenda mbele kuombea ili upate mkopo mpya.asante mungu siku hizi mabenk wanashirikiana ukidanganya tuu imekula kwako.
Wanaotaka watoto wao wafauluuuu na wewe umooooooo. Huna muda wa kuhimiza watoto kuwa na bidii ya masomo. Hujawahi hata kufuatilia homework zao. Hujui hata jina la mwalimu wake wa darasa japo akujuze mwanao anavyoendelea. Hata somo alilofeli hujui ni kwanini lakini uko mbele kuombewa ili wanao wafaulu mweeeeeeeeee.
Wanaosumbuliwa na wasichana wa kazi na wewe umoooooooo. Kwanza mshahara wake hujampa mpk leo eti unamtunzia? Kwanini usimfungulie akaunti ya benki kama ni kweli? Akivunja vyombo unamkata. Chakula unambagua. Dada wa kazi humpi muda wa kutoka na yeye akapumzike. Kutwa unawaza atatembea na mumeo. Akikosea unafoka asubuhi mpaka jion na kumpiga juu. Mkimaliza kula ndio dada wa kazi anakula kilichobaki. Watoto wako hutaki wamsaidie kazi mdada kwakuwa eti analipwa mshahara. Dada anakulelea watoto wako lakini unamtukana matusi makubwaa. Ukirudi huwezi hata kumletea zawadi dada anayekuchungia nyumba kisha umenyoosha mikono pale mbele eti wadada wa kazi wanakusumbua
Waliotupiwa mikosiiii na kulogwa watoke mbele niwaombeeeeee na wewe umoooooo. Kutwa unawaombea wenzio wapatwe na mabaya. Kila mama nanii akifanikiwa wewe unaumia. Huwezi hata kumshauri mwanamke mwenzako jambo la maendeleo eti asije kukupita. Mwingine akipendeza huwezi hata kumwambia kuwa kapendeza.
Wanaotaka wanaume zao wasiwasumbueeee na wewe umooooooo.* Wewe mwenyewe msumbufu tangu January mpaka December bado unataka mwanaume asikusumbue.?
Jiulize upo hapa duniani unafanya nini kama kila kitu mtu mwingine atakufanyia?
Mungu amekupa akili ili yaliyo ndani ya uwezo wako uyafanye na yale yaliyo nje yako umwambie mungu akusaidie.
Tuwapunguzie watumishi wa Mungu mizigo jamani na wao ni binadamu.