hsnaturalfertility
JF-Expert Member
- May 14, 2022
- 386
- 955
Imezuka tabia ya wahubiri vijana kuhubiri kwa kuchanganya kiswahili na kingereza (broken English) na tabia hii mimi binafsi inanifikirisha sana.
Kiufupi nikishajua muhubiri huyu ni mchanganyaji wa lugha huwa siwezi kumsikiliza hata nusu dakika. Sijui ndio ujanja au ndio waumini wanaelewa zaidi sijaelewa.
Ukweli ni kwamba mnaboa. Afadhali makanisa yenye wakalimani, angalau mtu unaelewa wanasema nini. Sasa unakuta mtu kingereza chenyewe cha huko Nyumbigwa halafu bado anakilazimisha mwe😭😭
Ushauri wangu, kama mnalenga waumini waelewe mnachofundisha ongeeni lugha moja, either kiswahili au kingereza, na kukiwa na ulazima basi tumieni wakalimani.
Asante sana.