aBuwash
JF-Expert Member
- Dec 26, 2023
- 260
- 491
Mimi ni mfanyabiashara wa nafaka hapa jijini Dar es Salaam. Sio mgeni katika kufanya biashara ila naweza sema ni mgeni katika kufanya biashara ya kwangu. Kwa sababu hapo awalii nilikuwa nafanya biashara za watu tuu.
Na sikujua kama biashara zina changamoto hivi hasa ukiwa wewe ndio mwenye biashara.
Mpaka sasa huu ni mwezi wa tatu nipo katika biashara yangu mpya ya nafaka nauza mchele na maharage nimepitia changamoto nyingi sana haswa matapelii, dalali kukutumia mzigo mbaya ambao unachukua kwa bei ya juu halafu ukifika sokoni lazima ukakate hela unauza bei ya chini kurudisha hela mda mwingine unaokoa tu hela. Changamoto ni nyingi kwakwelii ila sijakata tamaa napambana.
Sasa kuna hili swala.. ninapouza kuna jirani yangu naye anauza biashara kama yangu nimemkuta na inaonesha ana muda mrefu sana katika biashara, ana wateja wa kutosha na ana mtajii wa kutosha kiufupi kanizidii pakubwa sana.
Changamoto ipo kwenye wateja hivi wenzangu huwa mnahisi vipi mwenzako mmefungua duka sawa mna biashara zinazofanana ila chakushangaza mwenzako anauza gunia kumi asubuhi wewe ndo kwanza hata kilo moja hujauza 😁😁 mikokoteni inapaki kila muda plus mapikipiki muda wote hayakaukii yananunua mizigo pale wewe bado ngoma ngumuu.
Hivi wafanyabiashara wenzangu mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidiii kila kitu na ukizingatia wewe ndio kwanza unaanza ila miezi ndio hivyo mwezi watatu? Msaada wenu tafadhali
Nyongeza: Biashara ya mchele ni pasua kichwa sana walioweza sijui wanafanya vipi aiseee toka nimeanzaa faida siioni.
Nawatamani sana wateja wa jumla ila wanataka mchele mzuri halafu kwa bei mteremko bila kujua mimi nakochukua nachukua bei kubwa.
Swali lingine kwa wafanyabiashra wana mchele faida inabidi iwe sh ngapi kwa gunia kwa kawaida huenda mimi naweka faida kubwa halafu sijui.