Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,858
Katika kukabiliana na tatizo kubwa la wanafunzi wa vyuo vikuu kukosa mikopo,napendekeza zianzishwe tozo maalumu kwa ajili ya kutunisha mfuko wa Bodi ya Mikopo kwa lengo la kuwezesha watoto wa masikini kusoma vyuo vikuu bila kujali kozi wanazosoma au kiwango cha ufauli ili mradi mtu awe amepata admission katika chuo kinachotambulika na serikali.
Tozo hizo ambazo tunaweza kuziita HESLB zinaweza kutozwa katika maeneo yafuatayo:
Posho za watumishi serikalini
Posho zote zinazotambulika serikalini kama vile sitting allowance za wabunge,posho za majeshi,posho za watumishi wengine wa umma ambazo nazo hutolewa kila katika ya mwezi kama ilivyo kwa Polisi,Jeshi na Magereza,n.k, zinaweza kutozwa hadi asilimia 5 ya malipo ya mtumishi kwa kila mwezi na fedha hizo zikaelekezwa Bodi ya Mikopo.
Tukumbuke kuna kada hazina kabisa malipo ya aina hii zaidi ya kusubiri tu mwisho wa mwezi.
Malipo ya Huduma za Ving'amuzi
Ingawa tuliambiwa kuwa local channels za tv hapa nchini zitakuwa zinatolewa bure,ukweli ni kwamba hivi sasa tunalipia na hakuna anaefuatilia licha ya watu kuhoji juu ya swala hili.
Hivyo basi,TCRA watangaze rasimi kuwa channel za ndani nazo sasa zinalipiwa na hapo hapo itungwe sheria au kanuni ya kutozo asilimia 5 au zaidi kwa kila malipo yanafanyika kwa ajili ya kupata huduma hii ya ving'amuzi na mapato yaelekezwa Bodi ya Mikipo.
Faini za Makosa mbalimbali
Hizi ni pamoja na faina za makosa ya barabarani,faini za mahakamani, n.k.Hapa serikali inaweza kutoza hata asilimia 10 ya faini za sasa na pesa zitakazopatikana zikaelekezwa kusaidia kusomesha wanafunzi wa vyuo vikuu.
Kwa mfano asilimia 10 ya elfu 30,000 (faini ya makosa ya barabarani) ni sh 3000 hivyo sio haba japo makosa haya hayatakiwi kuwepo ila tukumbuke madereva nao hawataki kutii sheria na wanaangamiza maisha ya watu wengi pamoja na mali zao karibu kila siku iendayo kwa mungu.
Mauzo ya viwanja
Viwanja vinavyopimwa na kuuzwa na serikali nchi nzima vinaweza kutozwa asilimia hata 5 ya bei ya kiwanja na fedha zitakazokusanywa zikapelekwa bodi kwa ajili ya kugharamia elimu ya juu.
Kwa mfano, asilimia 5 ya kiwanja kimoja cha shilingi milioni 2 ni shilingi 10,000. Sasa kwa mwaka mmoja wa fedha kwa viwanja vya nchi nzima hela itakosekana hapo?
Ruzuku ya vyama vya siasa
Hii ruzuku inaweza kufutwa kabisa sambamba na sitting allowonce za wabunge na fedha zitakazookolewa zikaelekezwa bodi ya mikopo.
Vyama vya siasa havipaswi kuwa mzigo kwa mlipa kodi bali vianze kujiendesha vyenyewe na si kupewa ruzuku na serikali na hii itapunguza mnyukano wa kugombea na madaraka ndani ya vyama hivi na kuleta usawa katika ushindani wa kisiasa baina ya vyama hapa nchini.
Hata kama hatutapata fedha za kutosha kumaliza tatizo hili ila tutakuwa tumefanikiwa kulipunguza.
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchii hii wanateseka bure kwasababu tu hawajapewa kipaumbele na zaidi watu wamejaa ubinafsi lakini sio kweli kwamba serikali inashindwa kuwasomesha.