Hivi vigari vidogo vidogo vichafu vichafu vya zamani kama hasa IST na VITZ madereva vijana hawa wanafanya fujo sana barabarani

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,415
22,026
Katika kuendesha kwangu gari barabarani, nimegundua kwamba madereva wengi wa hivi vigari vidogo vidogo kama IST, wana fujo sana barabarani. Na mara nyingi utakuta ni vigari vichafu vichafu na vilivyochakaa.

Kila nikiangalia dereva wake, nakuta ni vijana wa kiume. Inaonekana wengi wao ni limbukeni ambao wamejibana matumizi hadi kuweza kununua kiji IST cha mtu fulani kakichoka, au wanaendesha gari za dada zao, na sasa wanajiona wao ndio wao, wamekuwa wanaume wa shoka barabarani. Hawana kabisa uvumilivu na ustaarabu wa barabarani. Wanapenda kutanua hata pasipokubalika kutanua, kila wakati ni fujo tu utafikiri wamevuta bangi ya Mufindi. Ukiwa barabara ukakuta gari za upande wa pili zimekwama mara nyingi ni hivi viroboto vimezuia njia. Huwezi kukuta dereva mstaarabu na gari yake safi kafanya ujinga kama huu, ni nadra sana.

Sasa tuwaambie ukweli, hivyo vi IST vyenu na vi VITZ vitawaua sana, nyie endeleeni kujifanya wajuaji wa barabarani. Kuna siku mtanikuta barabarani na mdude wangu fulani wa zamani wa mchanga nitawabamiza kwelikweli. Wee ngoja tu.
 
Back
Top Bottom