Hivi ushawahi kutetea/kuingilia ugomvi wa watu wengine?

Code 255

JF-Expert Member
Jul 6, 2024
904
3,559
Habari wana JF

Hivi kwenye maisha Yako ushawahi kujaribu kuingilia au kutetea ugomvi wa watu na nini kilikutokea?

Kwa experience yangu ya kutetea ugomvi nishawahi kukutana na changamoto tatu (3)zilizonifunza kutokuwa na kiherere kwenye mambo ya watu

1) Hii ilinitokea kipindi nipo mdogo.marafiki zangu walikuwa wanapigana.ile naenda kuwaachanisha mmoja si akakosea kurenga ngumi kwa adui yake ikanikuta ya jicho
Jicho likavimba,na nyumbani nikasemwa na mother Ile kinoma kwamba nachokoza watu wenye nguvu wakati siwawezi🥺🥺🥺

2)Hapa nishakuwa kijana wa makamo kabisa...tumeenda kuangalia mpira kibanda umiza. Rafiki yangu niliyeenda naye akaanza kubishana na jamaa aliyekaa jirani yake,si wakaanza kushikana mashati....Mimi na shobo zangu nikafika chapu kugombelezea,Ile ugomvi umeisha yule jamaa anasema ameibiwa simu na anasema mimi ndiye niliyechukua simu kwa kuwa nilimshika wakati nawaachanisha🤨🤨🤨

3 ) hapa nilikuwa nishapata funzo ya kushobokea ugomvi wa watu.....Kuna rafiki yangu si akaanzisha ugomvi halafu Hana nguvu......kumbe jamaa kichwani kwake anawaza Mimi nimtetee
Nilivyoona anaanza ujinga tu me nikainuka na kuanza kuondoka....nasikia ananiita "kaka unaenda wapi?nisubirie kaka"🤣🤣🤣

Vipi kuhusu experience Yako kwenye ugomvi wa watu??

1724568429653.jpg

 
Back
Top Bottom