Habari Gani wakuu
juzi(ijumaa) nimenunua umeme mida saa 12 jioni kupitia Tigo Pesa, kama ilivyo kawaida ukinunua umeme unaletewa ujumbe kwamba muamala wako umekamilika na majibu yakirudi unaletewa umeme(token)
maajabu nimepata juzi mpaka sasa bado yanaendelea kwanza waliniletea ujumbe ambao hawakuwahi kuniletea hata siku moja, ulisomeka hivi "Transaction successful" na manamba kibao bila token(namba za luku)
baada ya masaa 6 nilipiga simu huduma kwa wateja wakanambia kuna tatizo nikawaelewa, nililala kiza nikajua mpaka kufika asubuhi ya jana watakuwa washanitumia umeme, asubuhi kuamka hakuna kitu...nilivyowapigia bado wakanambia bado kuna tatizo, hivi mpaka sasa pesa yangu haijarudishwa na si kawaida yao kama kuna matatizo hurudisha pesa kama ilivyo.
maajabu zaidi yametokea leo baadhi ya watu wananunua umeme na baada ya sekunde 45 tu umeme wanapata.
sasa hapa nawauliza ndugu zangu na nyie pia iliwatokea au ndio nimelipia kodi bila kujua??
nimejiandaa na kila aina ya jibu
nawasilisha