Ni kama vile tokea atoke Kolokoroni pale Central Police huyu Msanii TID amezidi kuwa ni kama Mtu aliyechanganyikiwa. Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa sana interviews zake katika Media na Social Platforms zingine na kugundua kuwa athari za matumizi ya dawa za kulevya bado hazijamalizika kunako Ubongo wake.
TID amekuwa :
Mpayukaji
Mbwabwaji
Mkurupukaji
Hajielewi
Mpigaji mikelele hovyo
Analazimisha kujipendekeza
Mwongo
Kwa mnaomjua huyu Mtu kindakindaki nisaidieni je Jamaa bado anatumia au bado umegandiana hivyo inahitajika nguvu ya ziada kuweza kuuyeyusha utoke wote na arudi kuwa sawasawa?
Tatizo watu wanaomtumia wanamuaminisha kua amepona kwa kitendo cha kupanda pale jukwaani (ukumbi wa JK Nyerere) na kuongea kua yeye ni mla unga anaamini amepona ivyo analazimisha awe normal kumbe anaharibu.
Safari 1 Juma Mchopanga aliwahi kutahadharisha mwanzoni kabisa, "jamani, jamani, Mnyama anakula chakula cha Nyoka". Juma akaambulia diss kibao. Leo sasa Juma kakaa mbali analisoma movie kama hataki!