Hivi TCRA mnafahamu kuwa mtandao wa tigo unaibia wateja?

A JUSTMAN

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
439
555
Hii imenitokea sasa kwa mara ya pili ilishawahi kunitokea tena nimenunua vocha ya kiasi cha Tsh. 1500/- nimeongeza salio kwenye line yangu ya tigo, ajabu nataka nijiunge na kifurushi cha Tsh. 1500/- napata ujumbe mfupi kuwa "samahani salio lako halitoshi".

Napiga huduma kwa wateja naskitika sana sana sana sana sana .... kuambiwa eti nimejiunga na huduma ya sijui upuuzi gani unaitwa tigo hadithi, eti walinipigia simu na kuniuliza nijiunge nikakubali na kujiunga!
Kwanza naskia leo upuuzi unaoitwa tigo hadithi na sina mazoea ya kujiunga na huduma za kipuuzi kama hizo na hata simu yangu nayotumia hainiruhusu kujiunga humo.

HUU NI WIZI, NI UPUUZI, UTAPELI NA NI DHULUMA TIGO MNAFANYA KWA WATEJA.
MTAPOTEZA WATEJA KAMA MNAENDELEA NA WIZI HUU.

Leo mmeniibia kwa mara ya pili kwa mtindo uleule, sasa nahama tigo na pia nauliza TCRA ni kweli mnafahamu huu wizi unaofanywa na tigo?

 
Tigo ni wezi saaana!! Hata kama hujajiunga na chochote ukiweka salio ukakaa dakika tano ukiangalia unakuta wamepunguza.

Ukilala na salio kwenye simu ndo kabisaa wanajifanyia la kwao wanapunguza mpaka ubaki ziro kabisa!!
Inaskitisha sana na hii inaonekana wanafanya kwa kukusudia kabisa tena hata hawajali chochote na hawana wasiwasi kabisa jamani inakera sana yani
 
Je na salio la tigo pesa wanaiba?nauliza maana ndio nimeanza kuutumia
 
nimepigwa elfu 22 tigo pesa. Nimelalamika hadi nimeamua kusamehe maana nahisi mwishowe naweza kuvunja sheria buree.
 
Yani Tigo wanakera kweli na uwizi wao Wa aina hii wengi tu tunakatwa na hiyo huduma na ukiwapigia upate kujitoa custom care wanakupa menyu tofaut ya kujitoa sa sijui kunakamchezo kanacho endelea mi nna vocha za Tigo 2 kila nikiingiza naambiwa hazipo
 
Nadhani hili ni tatizo kwa mitandao yote... Ukiweka vocha hata usipoitumia utakuta imepungua au kuchukuliwa yote kabisa...
 
Hata mimi ningependa kujua namna ya kuzuia sms za matangazo zisiingie kabisa kwenye simu yangu.. msaada kwa anayejua..
 
wako biz na wanaomsema vibaya mtukufu, vingine fanyeni tu kwa buruuudani, wala hawana habari
 
Hivi nyie waheshimiwa, huwa mnakumbuka kuzima data kabla ya kuweka salio na kujiunga. Internet ikiwa inafanya kazi, pesa nyingine zinaliwa na data
hili halijawahi kukutoa ila likikutokea ndio utajua kama data ilikuwa on au off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…