Sister Abigail
JF-Expert Member
- Sep 2, 2020
- 2,867
- 9,010
Salaam,
Imenibidi niulize Kwa maana Hali Halisi niionavyo na nikiwa kama mhanga mmojawapo inanifkirisha sana. Nasema hivi sababu Kuna baadhi ya watu jinsi wanavyotendea wenye matatizo ya usikivu ni kama kuwafanya vituko. Hugeuza tatizo lao kuwa utambulisho badala ya kumsaidia.unakuta uko eneo lenye mkusanyiko anakufata mtu "choo Kiko wapi"?.. wakati unatarajia kumjibu anakuja au anadakia mtu "haskii vizuri"
Kwa Namna hii inakuwa anamnuong'onyeza yule mwenye tatizo badala ya kumsaidia. Hawa watu wako beneti mda wote attention kuhakikisha hakuna anaekuongeasha.hata salamu. Na hawa ndo wale wakishajua husikii vema basi hata salamu hakupi,anakupita kama sanamu hata ukimsalimia "habari yako" hakujibu. Mwingine unakuta ni Mzee kabisa,unatarajia atakuwa tofauti na labda sababu ya ukomavu kiakili lakini nae eti unamsalimia hajibu.nabaki naduwaa!.
Kuna wakati najiuliza matatizo ya sikio ndio makubwa kuliko yote,mbona mtu haoni vizuri anavaa miwani hafanyiwi hivi? Kuna watu bila miwani hawawezi hata kutembea barabarani,kusoma hawawezi kabisa,why hawapitii masaibu kama wenye usikivu hafifu?
Basi angalau iwe Kwa watu Baki,tunayapitia pia na Kwa tunaowaona wapendwa na ndugu zetu.maumivu yake sio madogo. Achana na ndugu na wapendwa Kuna nyumba ya ibada.nliwahi fanyiwa jambo nkajikuta nachukia kuingia nyumba ya ibada. Kwenye maofisi hasa ya umma Hadi tunaogopa.maana kama wenye masikio Yao tu wanakiona Cha moto vipi wewe mwenye masikio mazito🤣
Lakini pamoja na kukutana nawatu wenye kutibua hisia na maumivu,bado Kuna watu wema hata mie nakutana nao,ni watu waelewa,wako friendly hawajali kabisa ukiwa open unafurahia wanakusahaulisha hata shida zako..Mwenyezi Mungu awatunze sana!
Nb:Abigail ni muhanga wa Hilo tatizo na nilijua nko mwenyewe ama tuko wachache lakini nilivyojiunga kwenye jamii za wenye Hilo tatizo ndipo nkajua tupo wengi sana,asilimia kubwa ni vijana.japo vyanzo vya shida vinafanana na wengine havifanani,katika kushea changamoto wanazopitia nikaobserve mengi mojawapo ni Hilo.