Bila kuzungumzia account za kibenki ambazo compound interest somehow ipo applicable lakini lengo langu ni kuzungumzia kama kuna legally existing plan kwenye taasisi ambayo unaweza kufanya hichi kitu.
Yaani compound interest kwa maana ya kwamba gawio unalolipata automatically nalo linajijumuisha na kuwa sehemu ya uwekezaji wako.
Nimezoea wakati nasoma makala za fedha kwa nchi kama za US ama Euro utaskia kwamba wanazungumzia endapo mtu ataweka pesa yake mfano $10,000 katika fund ambayo inatoa compound interest ya labda 8% annnually na pesa hiyo ikakaa kwa miaka labda 30.
FV=PV(1+r)^n
=10,000(1+0.08)^30
=100,626
kwa hiyo kwa compound interest unakuta kwamba after 30 years account ya muhusika itakuwa na kama $ 100,626. Na nadhani kama sijakosea America wana hii kitu wanaiita 401k inawezekana ni mojawapo ya hizi compound interest schemes.
Ila kama ukichukulia mfano wa kibongo bongo ambapo hakuna well identified compound interest schemes in maana kwamba kwa $10,000 na kwa rate ya 8% ina maana total ambayo utakuwa nayo after 30 years ambacho umekusanya kwenye interest income ni $ 24,000.
Nadhani hapa sasa ndo taasisi zetu za benki na mashirika yetu ya pension yanapoanzia kuwapiga watu michanga ya macho. Hasa hasa hizi pension fund maana wao wanaishi na contributions za watu kwa zaidi ya miaka 35 so ideally ni kwamba wanakuwa wana enjoy hii compound interest effect na tumeona ni kiasi gani compound interest inavotoa faida kubwa. So sijui sasa kama pension wanazotoa zinalingana na faida ya kicompound interest.....
Maana am sure kabisa imagine mtu ulikuwa unaweka kama 200,000 na mshahara wako ni M1 kwa mwezi halafu ukaamua kwamba hiyo 200,000 uikusanye kwa miaka 10 ina maana utakuwa na kitu kama (200000*12*10=24,000,000) sasa baada ya kukusanya hiyo lumpsum nafanya assumption rahisi kwa kuangalia the average 15 year bond yield ambayo roughly nasema kwamba 12% though najua ipo zaidi ya hapo.
So ni kwamba sasa nasema kwa sababu ulitumia 10 years ku save ili upate hiyo lumpsum ya 24,000,000 so tuna assume umebakiwa na 25 years mpaka uje ustahafu. Ko sasa mahesabu yangu yanakuwa hivi.
Years 25
interest 12%
present value 24,000,000
Future value after 25 years= 24,000,000(1+0.12)^25
= 24,000,000(17.0000644)
Future value after 25 years= 408,001,546
Ko unaona sasa the effect of compound interest. Kama kungekuwa kuna scheme ya kueleweka ya compound interest ina maana mimi kwa mfano ningeweza tu kufanya kazi ama ka biashara changu halafu nika save 200,000 per month in ten years then nije niziweke hizo pesa kwenye compound interest na after 25 years unakuja ku resign na pension ya TZS 408,001,546.
So umeona compound interest ilivo na nguvu. Tuandamane serikali ifikirie hili swala.... Ndo mana nimeuliza kama huu mfumo upo? na kama haupo kwanini haupo?????