Katika kile ambacho kinaelezwa na serikali kuwa elimu ni bure kwa shule za msingi na sekondari bado kumekuwa na suntofahamu ya wazazi na walimu.
Wazazi wengi ambao wanafurahia tamko hilibla serikali, lakini bado kuna ukakasi.
Serikali imesema haitaki kusikia habari ya michango yoyote mashuleni, sio ada, dawati, mlinzi, mpishi, chakula, jembe, fagio, na vingine vingi.
Wakuu wa shule wengi kwa sasa wanaandaa join instruction kwa wanafunzi wa sekondari, lakini bado wanashindwa kuluweka suala la sare za shule kama sehemu ya mchango.
Kuna baadhi yao wanasema serikali itagharamia mpaka nguo za shule za wanafunzi.
Hivyo tunaomba serikali iweke wazi ni michango gani itagharamia na ambayo haitogharamiwa na serikali.
Nawasilisha.