Hivi pesa zipo Dar au mkoani?

Nadhani concern ya muulizaji ni kutaka kujua wapi atapata mishemishe zotazompa pesa kwa uhakika. Anyway labda sio hivyo lakin suala la upatikanaji pesa linategemea pia matumizi yake. Kuna mtu dsm anaweza pata pesa kirahisi sababu mzunguko wake mkubwa kwakuwa shughuli za kubadilishana pesa ni nyingi..kazi ipo NAMNA, WAPI NA WAKATI GANI UTAITEGA PESA, ila pia kuna mtu mkoani mahali pana fursa ya kupata pesa kama ya mtu wa aliye mjini akapata vizuri au kwa tabu kidogo lakini akaitumia vizuri zaidi kuliko wa mjini..so kote pesa zipo inategemea mhusika anatakeje. Mzunguko mkubwa wa pesa hauko kwenye kupata tu ni pamoja na kuitumia..speed na ufanisi wa kuitumia pesa uendane na kuitega japo kanuni inataka upate nyingi na kwa haraka na uitumie kidogo kwa Pole Pole..sasa kwa mjini ndo shida..kadri unavyopata ndivyo vya kukufanya uitumie vinaongezeka na kukuvutia...kama napata mchongo mkoani nitachagua huko
 
Back
Top Bottom