Utumwa huu utaisha pale tutakapoamua kwa hiari yetu kuvipenda vitu vilivyo zalishwa nchini mwetu. Unakuta mhehe naye ana kopo la Tomato sauce ya India wakati nyanya original zipo pale Ilula.
Tatizo, ni kwamba, wengi wetu tunajifanya tumekaa Ulaya na matembele tumesahau kuyala tunataka canned food, na wengine wanadhani wakienda kununua wali pale Shoprite wanaona watakuwa wamewaonyesha majirani zao kwamba nao wamepanda daraja.
La tatu, ni hili, upungufu wa ubora wa bidhaa zetu nao unachangia watu kupenda vya nje. Nadhani hata wewe ni shahidi, habari ya bidhaa za mchina. Hapa serikali ikisimamia suala la Viwango vya bidhaa zetu tunaweza kurudi kwenye msitari.