Hivi ni Rais gani mstaafu, amekuwa na ujasiri wa kukemea maovu ya CCM hadharani, zaidi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,843
31,053
Katika kumbukumbu zangu, hakuna Rais mstaafu wa nchi hii ameweza kuwa na ujasiri wa kukemea maovu ya CCM hadharani, zaidi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Mwalimu Nyerere alikuwa na ujasiri wa aina yake, hadi katika moja ya hotuba zake alidiriki kuwaambia CCM kuwa chama hicho siyo mama yake aliyemzaa hadi ashindwe kukihama!

Akaendelea kueleza kuwa yeye kama Binadamu mwingine hawezi kumkana mama yake mzazi aliyemzaa, lakini chama ambacho yeye ndiyo muasisi wake, anaweza kukihama!

Katika kuendeleza hoja zake, alieleza kuwa kama chama hiko, kikiacha misingi iliyoianzisha ya kuwajali wananchi wake wanyonge Kwa vitendo na badala yake ikawakumbatia matajiri pekee, atatangaza kukihama chama hicho mara moja.

Maneno hayo aliyatamka kabla hajafariki mwaka 1999, Kwa hiyo naamini kuwa endapo Mwalimu Nyerere, angekuwa hai hadi leo, angekuwa tayari amekihama chama hicho na kujiiunga na chama kimojawapo Cha upinzani, Kwa kuwa hivi sasa ndiyo chama hicho kimezidi kuwakumbatia Kwa nguvu zaidi, matajiri wa nchi hii na matajiri hao, wanajiona kama nchi hii ni yao peke yao na ndiyo wanaostahili kuitafuna keki ya Taifa peke yao!

Hii serikali ya CCM, haiwajali kabisa wananchi wake masikini na ndiyo inazidi kuwakamua Kwa Kodi mbalimbali.

Nimwombe Rais mstaafu aliyebakia hivi sasa, Jakaya Kikwete, asiwe mwoga na awakemee hao CCM, kutokana na maovu yao wanayoyafanya.

Mungu ibariki nchi yetu.
 
Ndiyo maana maccm yaliona ajabu sana Lissu alivyokemea rushwa ya uchaguzi huko Chadema, wao wamezoea kufumbia macho uchafu na ndiyo maana nchi inazidi kudidimia kazi wanayoweza ni Uchawa tu kumsifia Rais.
 
Katika kumbukumbu zangu, hakuna Rais mstaafu wa nchi hii ameweza kuwa na ujasiri wa kukemea maovu ya CCM hadharani, zaidi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
Raisi mstaafu kwa sasa ni mmoja tu, Kikwete. Kwelikweli, unategemea Kikwete amkemee Samia au serikali yake? Huyo huyo Kikwete alieambiwa Raisi Mstaafu na mke wake watakuwa wakipewa V8 mpya kila baada ya miaka 5 na allowance karibu 75% ya mshahara wa raisi aliyepo madarakani?

Ukitegemea atakemea basi kuna siku jogoo atazaa na bata!
 
Back
Top Bottom