Kwa kweli kaburi la demokrasia linazidi kuchimbwa. Wenye mawazo mgando wanafikri wapinzani wanakwamisha maendeleo, na kudhani kuwa maendeleo yataletwa na ile dhana ya kusifiwa sana, kushaniliwa na kukubaliwa kwa kila hoja wanazoleta kwa asilimia mia moja. Pasi upinzani, na wanajinasibu kwamba hawaoni upungufu wowote kwani akidi inatimia na miswada na bajeti vinajadiliwa na kupitishwa. Mi naamini kuwa mawazo mbadala kutoka upande mwingine so tu yana saidia kufanya marekebisho, Bali pia kuweka hali ya tahadhali na kutenda kwa umakini katika jambo ambalo hapo awali uliona ni thabiti na kamilifu.