Hivi ndivyo waislamu wanatofautina na vita vya gaza

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Apr 21, 2019
819
2,587
Waislamu wengi wanaumia sana juu ya Wapalestina wakitaka wasaidiwe, si mbaya, maana imeandikwa katika maandiko yao kuwa ndugu yako wa kwanza ni muislamu......

Lakini katika kupita huku na kule naona macho yao wanayaelekeza kwa Waarabu. Wakitaka Waarabu wachukue hatua dhidi ya Wazayuni. Nashindwa kuelewa why wawe Waarabu na si wao? Au Waarabu ndio wamiliki wa Uislamu au ndio sura ya kupigania haki?

Sahivi wanaisifia South Afrika kwa kuchukua msimamo wa kuilaani Israeli na kuishtaki ICC na wakati huo huo wana walaani Waarabu kwa kuwa kimya juu ya mzozo wa Gaza. Why wasiende wao kutoa msaada na si hadi Waarabu?

Waarabu sasa wao wapo bize kila siku kujenga nchi zao ziwe kama Ulaya na Marekani. Hawana habari na mizozo labda huenda ni sababu ya kushindwa mara kwa mara na Wazayuni. Au wameamua tu kugeukia maslahi ya nchi zao. Mfano Saudia Arabia, sasa wanajenga mji mkubwa wa kitalii wenye mandhari ya Newyork, Paris na London utakao kuwa na starehe za kila namna. Na isitoshe mwaka 2034 ndio watakuwa waandaaji kombe la dunia bila masharti ya kuingilia uhuru wa watu kama LGBTQ. Na pia inasemakane ufalme wa Saudia ni wakwe wa Wayahudi.

Maswali yangu

Je Waarabu ndio Uislamu?
Je Waarabu ni wasaliti?
Je Waarabu ndio wanapaswa kuwasaidia Wapelestina?
Je bila Palestina Uislamu haukamiliki?
Je ni Waislamu tu wa Wapalestina ndio wanaoteseka duniani?
Je ni nini wanachokitaka Waislamu hapo Palestina?

Na Jeff Massawe
 
Waarabu wamewasaidia sana waarabu wenzao huko Gaza Judea na Samaria na wanaendelea kiwasaidia but zile njemba hazina fadhira ndio tatizo lao.. ukisaidia wanaona ni haki yao na ukiacha wanakutusi na dhihaka.. sasa wanaanzisha vitabwenyewe and wanawalaumu nchi saidizi pumbavu sana Iran aliona wanalilia Wembe wanyoe vuzi akawapa ndio wamejichana bandeji hamna damu inamiminika
 
Uislam sio Uarabu.

Hiyo sio vita ya kidini ni siasa na maslahi.
Huusiano wa imani, ukaribu geography na uchumi wa nchi za kiaarabu

waislamu wanaona kuna namna hao jamaa wanatakiwa wafanye kitu kikubwa wanasahau kuwa Israel ni US asset, arab nation ni US puppets. Hawana uwezo huo kwa sasa

Angalau.mika ya nyuma kulikuwa na strong arab leaders. Wote wameuawa
 
Waislamu wengi wanaumia sana juu ya Wapalestina wakitaka wasaidiwe, si mbaya, maana imeandikwa katika maandiko yao kuwa ndugu yako wa kwanza ni muislamu......

Mkuu:

Wengi ukiwaambia adui mkubwa wa Waarabu ni Waarabu wenyewe, kwanza swala la Wapelestina, Waarabu wanalizungumza mdomoni tu.....Toka awali, huko nyuma enzi za akina Yasser Arafat wamekuwa na misimamo tofauti tofauti, Nakupa nukuu ya kiongozi wa Wapelestina rnzi hizo, Zuheir Mohsen, yeye alisema wazi hakuna taifa la Wapelestina, wamelitengeneza tu Waarabu kuipigana na Israel....

"The Palestinian people does not exist. The creation of a Palestinian state is only a means for continuing our struggle against the state of Israel for our Arab unity. In reality today there is no difference between Jordanians, Palestinians, Syrians and Lebanese. Only for political and tactical reasons do we speak today about the existence of a Palestinian people, since Arab national interests demand that we posit the existence of a distinct 'Palestinian people' to oppose Zionism."

QUOTES BY ZUHEIR MOHSEN

Egypt ilifunga mpaka wake na Gaza toka 2005, Mpaka leo! Haitaki kabisa kusikia Wapelestina wanaingia huko.... Na baada ya OctoBER 7 Wamejenga ukuta kabisa....! Wanaposema Gaza ni jela ya nje......Ujue sio Israel tu imewaweka kifungoni......Hata Egypt pia......Na kila nchi ina sababu zake! Rudia historia uone Jordan iliwafanyia nini Wapelestina!

"Since the war between Israel and Hamas erupted on Oct. 7, Egypt constructed a concrete border wall that reaches six metres into the ground and is topped with barbed wire. It has also built berms and enhanced surveillance at border posts, the security sources said."

Source: Reuters
 
Duh hatari sana
 
Waarabu siyo waislam,wapalestina siyo waislam,wazungu siyo waislam, waafrika siyo waislam na kadhalika...

Ila waislam wanaweza kuwa ni waarabu, waafrika, wapalestina,wazungu na kadhalika.

Uislam utatetea kila uonevu na umwagaji damu kokote duniani pasi na kuangalia ni Race Gani inaonewa na damu yake inamwagwa bila Haki.
 
Vip

Hapo Darfur Sudan waarabu wanawaua waafrica waislamu umewah hata kufungua uzi humu kuumia kwaajili yao mkuu?
 
Waislamu wa Sudani Kusini walipokuwa wanauwawa na Waarabu Wasudani.

Hakuna Mwafrika yoyote aliye wahurumia.

Leo tunawalilia Wapalestina kwakuwa ni Waislamu wenzetu.

Je sisi Waislamu wa Afrika yakitukuta majanga ya kuawa, hao Wapalestina watatulilia kweli ?

Mbona Wapalestina hawakuwalilia Waislamu Waafrika wa Sudani Kusini walipokuwa wanauwawa?
 
Waislam wanawalilia kila watu wenye kuonewa duniani siyo tuh wasudani,ni dhambi katika Uislam kuua kiumbe chochote kisicho na hatia...hata hao wapalestina wanaouawa siyo wote ni waislam,wapo wapalestina wanaoamini Imani zingine pia waislam wanawalilia bila kutazama Imani Zao
 
tueleze, uislam umeteteaje mauaji na ethnic cleansing ya Sudan inayoendelea sasaivi waarabu wa sudan wanapowafuta waislamw weusi? uislam ni dini moja ya kinafiki sana.

tukija kwenye suala la middle east, kinacholindwa pale ni msikiti wa al aqsa na mji wa yerusalem, kama hivyo visingekuwepo nakuhakikishia wapalestina wangesha assimilate kwenye mataifa mengine yanayowazunguka. hiyo ni vita ya kidini pure, tusimung'unye mambo. ndio maana hata waislam wengine kokote kule waonewe hawasaidiwi ila ukigusa lile eneo utafikiri umewagusa sehemu za siri. angalia mfano, stateless people wa rohinya, wale jamaa wanateseka kuliko chochote, na kila wanakoenda wanatengwa mojawapo ya sababu ikiwa ni kwasababu ya uislam wao, imagine mtu anakutenga kwasababu ya imani yako wakati na yeye anayo ya kwake. waislam hawawasaidii wala nini, hakuna cha pakistan wala indonesia, indonesia ndio kawafukuzia mbali labda kwasababu wana visura kama vya kihindi kwa mbali. ukija sudan, zaidi ya watu 5m wamefukuzwa wanalala maporini ila gaza hata 2m hawafiki, ila waarabu wanapaona gaza tu. unafiki mtupu.
 
Islaeri Inabidi ijilinde Kweli ingekuwa Dhaifu Nahisi Wapalestina Wange Fanya Kila wanacho taka kibaya Na kutamba Wao Ila Sasa Islaeri ina Power na Tulivu Sanaa huoni akipigana Na Nchi Nyingine Bila Sababu huo ndio utofauti.
 
Israel lazima ipigane na hizo nchi za kiarabu sababu hilo ndio lengo la hila taifa kiwekwa hiyo position,

Israel ni military base. Hiyo ndio main purpose. Hayo mengine ni kelele tu.
Kuna wapelestina kibao wana Uraia wa Israel na familia zao ni blood relative wengine wanaishlhi na kufanya biashara ndani ya Israel.

Hila media haziwezi kukuambia sababu ya ya boost hostility na kutafuta justification ya huo mgogoro

Jews vs zionist

Jews hawana shida na waarabu utawakuta wapo kwenye nchi kibao za kiislamu na kiaarabu.

Zionist ndio tattizo, kuna maandamano na harakati nyingi za jews kujaribu kujiweka mbali na zionist hila ndio ngumu zionist ndio wameshika mpini, jews wanatumika kupush agenda isiyo wahusu

Hapo gaza kuna mafuta na gas ya kufa mtu, watu wanaitaka
 
Waislamu wa Sudani Kusini walipokuwa wanauwawa na Waarabu Wasudani.

Hakuna Mwafrika yoyote aliye wahurumia.

Leo tunawalilia Wapalestina kwakuwa ni Waislamu wenzetu.

Je sisi Waislamu wa Afrika yakitukuta majanga ya kuawa, hao Wapalestina watatulilia kweli ?

Mbona Wapalestina hawakuwalilia Waislamu Waafrika wa Sudani Kusini walipokuwa wanauwawa?
unamlilia mtu mpk wengine wamlilie ? ukiitwa zuzu utakataa?
 
Waarabu wamewasaidia sana waarabu wenzao huko Gaza Judea na Samaria na wanaendelea kiwasaidia but zile njemba hazina fadhira ndio tatizo lao.. ukisaidia wanaona ni haki yao na ukiacha wanakutusi na dhihaka.. sasa wanaanzisha vitabwenyewe and wanawalaumu nchi saidizi pumbavu sana Iran aliona wanalilia Wembe wanyoe vuzi akawapa ndio wamejichana bandeji hamna damu inamiminika
Waparestina sio wote ni waarabu lakini pia sio wote waislamu makinka na hilo
 
Back
Top Bottom