Haijawahi kukutokea kutamani kuwa na akaunti zaidi ya moja za Facebook, Whatsapp, Instagram na Messenger katika simu moja? Hujawahi kutamani kuwa na akaunti zaidi ya moja katika tovuti zinazotoa huduma za kucheza magemu?
Kuna njia nyingi sana katika mitandao za jinsi ya kuwa na akaunti zaidi ya moja za mitandao ya kijamii katika simu zetu, lakini nyingi ni ngumu kutumia na zinahitaji uwe na uelewa mkubwa wa mambo ya simu. Moja ya njia zilizobamba sana katika mitandao za jinsi ya kuweka Whatsapp mbili katika simu moja ni pamoja na ile ya kutumia
OG Whatsapp ambayo unaweza ukaipata hapa.
Lakini leo naomba nikupe njia rahisi na ya haraka ya kufanya hivyo, tena inatumika kwa mitandao yote ya kijamii na ya kucheza magame online. Hii si nyingine bali ni application ya
Parallel Space, ambayo inapatikana kwenye
Google Play na kwenye mtandao wao.
Parallel Space inakupa uwezo wa kufanya yote hayo bila hata ya kuroot simu yako ya android, hii itakusaidia sana kama una simu zetu hizi za kisasa zinazotumia laini mbili (Dual SIM) na ungependa zote ziwe zimeunganishwa katika mitandao uipendayo.
Baada ya kuidownload (Pakua) na kuinstall application hii unachotakiwa kufanya ni kuifungua na kubonyeza alama ya Add ili kuweka application nyingine. Njia zote zinazofuata ni kama uinstall application hizo kwa kawaida.
Parallel Space inahitaji uwe na simu yenye toleo la Android kuanzia 4.0.3 na kuendelea na kwa sasa application hiyo ina ukubwa wa MB 2.9.