Hivi mtu anajisikiaje anapojitambulisha kuwa na elimu kubwa halafu uwezo wake ukawa mdogo kuliko mwenye elimu ndogo?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,260
Sijui watu wa aina hii wanajisikiaje wanapojitambulisha kuwa na elimu kubwa kama Phd, Uprofesa, Uinjinia na ubobevu katika masuala fulani halafu kiutendaji, uelewa wa mambo, busara, hekima na lugha wanakuwa chini sana kulko wenye elimu ndogo mathalani ya darasa la saba, sekondari au hata digrii moja. Nikiangalia baadhi ya viongozi wetu wanapenda sana kujionesha kuwa ni wasomi lakini kusema kweli ni majina tu lakini uwezo ni mdogo sana. Katika nchi nyingi sana duniani ikiwemo zile zilizoendelea kiuchumi na kiteknolojia huwezi kukuta viongozi wao wakijitambulisha kwa vyeo vyao vya kielimu za kusoma na kupewa kama Dr, Prof, Eng, nk lakini wabongo wanavyopenda sifa! Ukijitambulisha kwa elimu kubvwa lazima watu waone uwezo wako kivitendo, hekima na busara.

Ingekuwa vizuri sasa wapenda sifa hao wawe wanaweka kabisa CV zao zikionesha jinsi walivyofaulu huko shuleni na vyuoni. Mfano kiongozi aweke wazi matokeo yake ya Sekondari Kidato cha nne na sita tuone ufaulu wake katika kila somo alipata nini. Vile vile katika ngazi ya chuo kikuu na vyuo vingine aweke Transcript yake tuone alifanya nini na alipata Class gani. Tukifika kwenye Phd na Uprofesa pia tuone walibobea katika nini na walipataje kufika ngazi hizo kama vigezo na masharti vilizingatiwa. Tukifikia hapo huu ujanja ujanja wa kujiita Dr, Prof. na Eng, utaisha. Ukiwaangalia VP na PM utagundua wako vizuri sana kulinganisha na wenye mikwara ya uprof na Phd. Hotuba zao huwa zinakuwa za kitaifa zaidi bila ubaguzi wala kuleta mitafaruku huwa wanajitahidi sana kutenganisha shughuli za kiserikali na chama na huwa wametulia sana
 
Mkuu acha hizo habari za kujadili elimu za watu
Utani kama huo mpaka leo Eight O'clock hatumuoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Obama na Angel Merkel ni maprofesa ila Obama alikuwa anaitwa Mr President
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Obama na Angel Merkel ni maprofesa ila Obama alikuwa anaitwa Mr President

Sent using Jamii Forums mobile app
Huku kwetu mtu hata akiukwaa udoka wa njia ya mkato wa maganda ya maharage basi ni shida tupu kila mahali ni Dr Dr yaani kana kwamba hakuna madokta wengine isipokuwa yeye. Sasa njoo kwenye uwezo na kujieleza ndipo utachoka!
 
Tatizo wajinga wengi mlipenya kwenye nafasi za kisiasa na sasa mnaisi ulaji unaishia. Unawezaje kusema MTU ni msomi halafu uwezo mdogo. Pathetic
 
Kwanza lazima uelewe huyo mjinga ni mzingo kwa wengine na hapo hajijui katika ujinga wake....ila anawapa tabu tuu wengine
 
Angalia pia asili ya ya mtu. Wenye hizo sifa iliotaja, ukiachilia uanasiasa, je ni wa asili ya wapi? VP na PM nao kwa upande mwingine ni wa asili ya wapi? Hapo utaona tofauti inayotokana pengine na malezi, mila na desturi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Dr. Profesa Engineer Tulimumu. Tumekupata na tutaufanyia kazi huu ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…