Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 92
- 1,684
Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.
1. Pengine utasema ni kahaba kwasababu kavaa nguo fupi sana dizaini ya chupi au nyinginezo.
Lakini hii sio ushahidi wa mtu kuwa kahaba. Tanzania hatuna Sheria inayoelekeza(regulate) mavazi. Mtu anaweza kuvaa vyovyote vile. Na pia hakuna mavazi mtu akivaa anahesabika kahaba kwa mujibu wa sheria.
2. Pengine utasema nimemkuta amesimama sehemu fulani usiku wa manane.
Kusimama nje usiku wa manane sio ushahidi wa ukahaba/ biashara ya ngono. Wengi wetu husimama na hatufanyi hizo biashara.
Pia Tanzania hakuna kosa mtu kusimama sehemu yoyote usiku wa manane labda sehemu hiyo pawe panazuiwa kusimama na mmiliki wa pale.
Na kama mmiliki wa pale ndio hapendi mtu asimame basi hiyo sio kesi ya mkuu wa wilaya bali ya mmiliki dhidi ya aliyesimama pale. Na so far sio kesi ya ukahaba bali uvamizi wa eneo(trespass).
Kusimama nje ya Baa, nje klabu, nje ya kituo cha mabasi kama Riverside, au kurandaranda nje tu, au kuwa popote nje usiku sio kosa na sio ushahidi wa kufanya biashara ya ngono. Watu kada zote husimama maeneo hayo.
3. Pengine utasema nimemkuta lodge, guest nk. Tena akiwa na mwanaume au wanaume.
Kuwa lodge,guest na mwanaume, wanaume, au peke yako sio ushahidi wa ukahaba.
Hope hata huyo mkamataji amewahi mara kadhaa kuwa maeneo kama hayo na hakukamatwa kwa kushiriki ukahaba.
Na zaidi, mwanamke kuwa ndani ya lodge au guest peke yake au na mwanaume au wanaume(3 au 4s..me) nalo sio kosa Tanzania, na hata iwe usiku wa manane ama mchana kweupe.
4. Pengine utasema nimemkuta kwenye vile vijumba wanavyopanga vya uwanja wa fisi na mwananyamala.
Si atasema mi naishi hapo. Na hata kama umemkuta na mwanaume au wanaume atasema ndio nilikuwa nao sasa kosa liko wapi. Kuwa na mwanaume au wanaume nyumbani kwangu linakuwaje kosa nchi hii. Hata ukiwakuta wanafanya kosa liko wapi, si nchi nzima ingeishia jela kama ni hivyo.
5. Ushahidi wa Ukahaba/biashara ya ngono.
Kitu pekee kinachoweza kuthibitisha kuwa mtu fulani anafanya biashara ya ngono na mtuhumiwa akapatikana na hatia bila wasiwasi ni kimoja tu. Ni mtuhumiwa mwenyewe kukubali kuwa ni kweli anafanya biashara hiyo.
Anyway, tusiseme sana lakini hili jambo ni gumu .
Namuona Mkuu wa Wilaya akiwalipa fidia ya udhalilishaji hawa viumbe.
Tunaongelea SHERIA hatutetei wala kumkandamiza yeyote.
PIA SOMA
- Vita ya DC Ubungo na Makahaba: Mgongano wa sheria, haki na maadili
- Mkuu wa Wilaya ya Ubungo adhamiria kutokomeza biashara ya ukahaba